Trump ameongeza ushuru huo siku moja tu baada ya Israel kutangaza kuondoa ushuru wote kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka Marekani.
Wachambuzi wa mambo wanaamini kuwa utawala wa Israel ulichukua hatua ya kupunguza kutoza ushuru bidhaa kutoka Marekani ikitumai kuwa Marekani nayo itaupunguzia ushuru utawala huo.
Hata hivyo, maafisa wa Israel wameshtushwa kusikia kwamba serikali ya Marekani si tu imekataa kuondoa ushuru kwa bidhaa za Israel zinazoingia nchini humo bali imekwenda mbali zaidi na kuzidisha ushuru kwa bidhaa zinazotoka kwa utawala wa Kizayuni.
Amichai Stein mwandishi wa habari wa utawala wa kizayuni amesema wameshtushwa na uamuzi huo wa Marekani."
Inafaa kuashiria hapa kuwa, biashara kati ya Marekani na Israel ilifikia dola bilioni 34 mwaka jana nwa 2024, huku Marekani ikiwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa utawala huo ghasibu.
Kuongezewa ushuru kwa bidhaa za Israel ni sehemu ya tangazo kubwa la ushuru la la Trump kwa jina la " Reciprocal Tariffs" ambalo limejumuisha viwango vya ushuru kwa nchi zote duniani.
342/
Your Comment