Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Algeria, "Algeria siku ya Jumatano iliomba kuitishwa mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama kuhusu hali ya Palestina, na kikao hicho kinatarajiwa kufanyika Alkhamisi mchana."
Shirika hilo la habari limedokeza kuwa, ombi hilo liliwasilishwa kutokana na "ongezeko kubwa (la mashambulizi ya Israel) katika maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu, hasa Gaza, ambayo imekuwa katika mzingiro kwa zaidi ya mwezi mmoja, ikiambatana na mauaji ya kiholela, yakiwemo ya wafanyakazi wa utoaji wa misaada."
"Ombi hilo pia linakuja kufuatia tangazo la kupatikana miili 15 ya wafanyakazi wa dharura na wa misaada huko Gaza, wanaohusishwa na shirika la Hilali Nyekundu ya Palestina, Ulinzi wa Raia wa Palestina, na Umoja wa Mataifa," limeongeza.
Rais Abdelmadjid Tebboune wa Algeria ambaye ni katika watetezi wakubwa wa Palestina
Ombi hilo la Algeria pia linakuja "kutokana na kuongezeka kwa ghasia za walowezi katika Ukingo wa Magharibi."
Algeria ni mwanachama asiye wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, pamoja na nchi nyingine 14, zikiwemo nchi tano wanachama wa kudumu: Marekani, Uingereza, Ufaransa, China na Russia.
Israel ilianzisha hujuma mpya za anga huko Gaza mnamo Machi 18, ambapo mpaka sasa imeua zaidi ya watu 1,000 na kujeruhi zaidi ya 2,500, mbali na kuvunja makubaliano yake na Harakati ya Muqawama ya Palestina Hamas ya Januari ya kusitisha mapigano na kubadilishana wafungwa .
342/
Your Comment