4 Machi 2025 - 23:36
Source: Parstoday
UNICEF yaonya Israel dhidi ya kuzuia misaada kuelekea Gaza

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF limeonya kuwa uamuzi wa Israel wa kuzuia upelekaji wa misaada ya kibinadamu isipokuwa maji kwenye Ukanda wa Gaza, kwa haraka utapelekea hatari kubwa kwa watoto na familia ambazo tayari zimetatizika.

“Kusitishwa kwa upelekaji wa misaada kulikotangazwa Jumapili kutaathiri pakubwa operesheni za raia,” amesema Eduoard Beigbeder, mratibu wa kieneo wa UNICEF kwa ajili ya Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika.

Aidha ameongeza kuwa, “ni muhimu usitishaji viita kuendelea kuwepo, pamoja na kuruhusiwa upelekaji wa misaada ili tuweze kuendelea na shughuli za kibinadamu,” Beigbeder amesema.

Hatua ya Israel ya kuzuia kuingizwa misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza imelaaniwa na Misri na Saudi Arabia, huku nchi mbili hizo zikisisitiza kuwa kitendo hicho ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa.

Kabla ya hapo, Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina ililaani pia uamuzi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wa kuzuia misaada ya kibinadamu kuingia Gaza na kuonya juu ya madhara ya hatari ya hatua hiyo katika mgogoro wa sasa hususan katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Kadhalika Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imelaani vikali uamuzi wa utawala wa Kizayuni wa kuzuia misaada ya kibinadamu kuingia Gaza na kufunga vivuko vyote vya Ukanda wa Gaza.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha