5 Machi 2025 - 22:38
Source: Parstoday
Viongozi wa Ulaya waumizwa na kusitishwa msaada wa kijeshi wa Marekani kwa Ukraine

Uamuzi wa Marekani wa kusita kuipa Ukraine silaha umepata majibu tofauti kutoka kwa viongozi wa nchi za Ulaya.

Rais wa Marekani Donald Trump amesitisha msaada wa kijeshi kwa Ukraine baada ya kurushiana maneno na mwenzake wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy wiki iliyopita.

Leonid Slutsky, Mkuu wa Kamati ya Masuala ya Kimataifa ya Duma la Russia amegusia uamuzi wa Marekani wa kusitisha msaada wa kijeshi kwa Ukraine na kusema: "Sasa ukurasa mwingine mweusi umeandikwa katika rekodi ya Zelenskyy baada ya kutimuliwa na Trump katika Ofisi ya Oval ya Ikulu ya White House."

Mbunge huyo wa Russia amezungumzia pia mkutano wa hivi karibuni wa viongozi wa Ulaya mjini London na ahadi zao na kuwatanabahisha viongozi wa Kyiv akiwaaambia: "Msidanganywe na ahadi za Wazungu wanaodai kuwa wataendelea kukusaidieni madhali mnaendelea na vita."

Kwa upande wake, Kansela wa Ujerumani Olaf Schulz, amezungumzia tangazo la Waziri Mkuu wa Uingereza kuhusu mpango wa kuunda muungano mpya wa kuiimarisha Ukraine katika vita dhidi ya Russia na kudai kuwa usalama wa Ulaya unategemea Ukraine yenye nguvu. Lakini kansela huyo wa Ujerumani hakusema kama Berlin itapeleka wanajeshi wake Ukrain au la. 

Nayo wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa imelalamikia uamuzi wa Marekani wa kuacha kuipa silaha Ukraine kuanzia jana Jumanne. Benjamin Haddad, mkurugenzi wa masuala ya Ulaya katika wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa amesema katika mahojiano maalumu na redio moja kwamba: "Ikiwa kweli tunataka amani, basi uamuzi wa kuacha kupeleka silaha Ukraine utachelewesha amani."

Marekani ndiyo hasa iliyowachochea viongozi vibaraka wa Ukraine kuingia vitani na Russia, lakini sasa wamewaacha mkono na kuwadhalilisha vibaya ikiwa ni pamoja na kutimuliwa rais wa Ukraine katika Ikulu ya Marekani, White House, hivi karibuni.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha