Mwandishi wa IRIB amemnukuu Meja Jenerali Abdul Rahim Mousavi akisema hayo wakati alipozungumzia mafanikio ya mazoezi ya pamoja ya kijeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yanayojulikana kwa jina la Zulfiqar ambayo yamefanyika tena baada ya kusimama kwa mwaka mmoja.
Katika luteka hiyo ya kijeshi ya takriban wiki nzima, vikosi vinne vya jeshi vilifanya mazoezi ya kijasusi, vita vya msituni, kujihami n.k. Mazoezi hayo yalimalizika Jumanne iliyopita.
Akizungumzia mafanikio ya luteka hiyo, Meja Jenerali Mousavi, Kamanda Mkuuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, tumewaonesha maadui kwamba nguvu zetu zimeongezeka. Hatutaki vita lakini tumejiaandaa kujihami na kulilinda taifa letu kwa nguvu zetu zote.
Akihojiwa na mwaandishi wa IRIB, Meja Jenerali Amir Mousavi amesema: Lengo kuu la mazoezi hayo lilikuwa ni kupima uwezo wa kivita na utayari ambao umeongezwa ndani ya jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Mbali na mafunzo, mabadiliko ya mazingira na vitisho, silaha na vifaa ambavyo vimebuniwa na wanasayansi wa nchi yetu ndani ya viwanda vya silaha na mashirika ambayao msingi wake ni elimu, navyo vimefanyiwa majaribio kwenye luteka hiyo.
Katika asehemu nyingine ya mahojiano hayo, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, kuna matukio mengi yametokea katika kipindi cha miezi 16 hivi au zaidi, na huenda maadui zetu wakajipa uthubutu waa kufanya makosa katika maamuzi yao dhidi yetu. Kwa hivyo ilibidi tuwaoneshe kuwa nguvu za kivita za Iran zimeongezeka ikilinganishwa na miezi mitano au mwaka mmoja uliopita.
342/
Your Comment