7 Machi 2025 - 22:28
Source: Parstoday
Iran yateuliwa Makamu wa Rais wa OPCW licha ya upinzani wa Marekani

Iran imechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Baraza la Utendaji la Shirika la Kuzuia Silaha za Kemikali (OPCW) licha ya Marekani kufanya juu chini kuzuia Jamhuri ya Kiislamu kuteuliwa kwenye nafasi hiyo.

Uchaguzi huo ulifanyika wakati wa kongamano la kila mwaka la taasisi hiyo ya serikali za dunia inayosimamia juhudi za kimataifa za kutokomeza kabisa kwa silaha hizo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Mehr, Iran imeshinda kiti hicho katika Kikao cha 108 cha Baraza la Utendaji la OPCW huko mjini Hague nchini Uholanzi.

Marekani ilikuwa imejaribu kuzuia ombi la Iran katika baraza hilo kupitia mashinikizo kwa wanachama wa Jumuiya ya Kuzuia Silaha za Kemikali (OPCW).

Baraza Kuu linajumuisha nchi 41 wanachama wa OPCW ambazo huchaguliwa kwenye Mkutano wa Nchi Wanachama na huzunguka kila baada ya miaka miwili.

Baraza hilo linasimamia shughuli za Sekretarieti ya Kiufundi na lina jukumu la kukuza utekelezaji mzuri na kuheshimiwa Hati ya jumuiya hiyo ya kimataiifa.

Ili kuhakikisha ufanisi wa Baraza la Utendaji, Hati ya jumuiya hiyo inataka uanachama uundwe kwa kuzingatia kanuni ya ueneaji sawa wa kijiografia, umuhimu wa sekta ya kemikali, na maslahi ya kisiasa na kiusalama.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha