Uchunguzi huo uliofanywa na gazeti la Uingereza la The Guardian na matokeo yake kutolewa jana Alhamisi, umeshirikisha pia jarida la +972, na kituo cha lugha ya Kiebrania cha Local Call.
Uchunguzi huo umeeleza bayana kuwa, Kitengo cha 8200 kilifunza kifaa hicho cha AI kuelewa Kiarabu kinachozungumzwa, kwa kutumia idadi kubwa ya mazungumzo ya simu na ujumbe wa maandishi, unaopatikana kupitia ufuatiliaji wake wa kina wa maeneo yanayokaliwa kwa mabavu.
Kitengo hicho cha kijasusi kiliharakisha uundaji wa chombo hicho baada ya kuanza kwa vita vya mauaji ya halaiki ya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza mnamo Oktoba 7, 2023 na kutoa mafunzo kwa nusu ya pili ya 2024, uchunguzi ulibaini, na kuongeza kuwa, haijabainika ikiwa modeli hiyo bado imeshatumiwa na jeshi vamizi la Israel.
Nadim Nashif, Mkurugenzi wa kikundi cha haki za kidijitali cha 7amleh amesema Wapalestina "wamekuwa wahanga katika maabara ya Israel ili kuendeleza mbinu hizi na kumiliki silaha za AI, yote hayo kwa madhumuni ya kuubakisha hai utawala huo wa kibaguzi na ghasibu."
Huko nyuma pia, tovuti ya habari ya ICAD ilifichua kuwa, utawala wa Kizayuni unawafanyia ujasusi mkubwa watumiaji Waarabu wa mitandao wa kijamii ikiwa ni pamoja na kudukua mambo wanayoyatuma kwenye mitandao hiyo ili kupata watu wa kuwatumia kwa maslahi yao.
Mashirika ya kijasusi ya utawala wa Kizayuni yametenga fedha nyingi za kuwarubuni na kuandaa rasilimali watu kwa ajili ya kuwatumia kwenye masuala ya kijasusi.
342/
Your Comment