9 Machi 2025 - 22:03
Source: Parstoday
Korea Kaskazini: Tutatoa jibu kali kwa maneva ya kijeshi ya Korea Kusini na Marekani

Korea Kaskazini imeionya Seoul na kutishia kuchukua hatua kali iwapo mazoezi ya pamoja ya kijeshi ya kila mwaka kati ya Korea Kusini na Marekani yataendelea katika wiki zijazo.

Pyongyang imesema kuwa, Korea Kusini na Marekani zitagharamika pakubwa kwa maneva hayo ya kijeshi. 

"Nchi maadui zitalazimika kulipa gharama kubwa kwa maneva yao ya kijeshi ya kipumbavu ambayo yatapelekea Korea Kaskazini kuchukua hatua za haki za kujihami", imesema taarifa ya Pyongyang 

Pyongyang imetoa onyo hili siku mbili baada ya Korea Kusini na vikosi vya jeshi la Marekani kutangaza kuwa mazoezi ya kijeshi yaliyopewa jina la "Ngao ya Uhuru" yataanza Jumatatu ijayo na kuendelea kwa siku 11. 

Pyongyang imeyalaumu majeshi ya Seoul na Washington kwa maneva hayo na kusisitiza kuwa iwapo Marekani itaendelea kutunisha misuli kijeshi, Pyongyang pia haitakuwa na chaguo jingine ghairi ya kuhuisha uwezo wake wa kukabiliana na hujuma za adui.

Korea Kaskazini, kwa muda mrefu sasa, imekuwa ikishutumu na kukosoa mazoezi ya kijeshi ya Marekani na Korea Kusini na kuyataja kuwa yana lengo la kutekeleza hujuma na uvamizi. 

Kim Yo-Jong, dada wa Kim Jong-un Kiongozi wa Korea Kaskazini, wiki iliyopita alikosoa kuwasili meli ya kubeba ndege za kivita ya Marekani, USS Carl Vinson, na kushuhudiwa harakati nyingine za kijeshi za nchi hiyo katika kambi ya jeshi la wanamaji la Korea Kusini huko Busan. 

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha