Pars Today, imelinukuu Shirika la Habari la Wanachuo wa Iran (ISNA) na kuripoti kuwa, shakhsia kadhaa wa kijeshi na kisiasa wa Iran wametoa maoni yao kuhusu masuala mbalimbali ya kimataifa katika mahojiano waliyofanyiwa na chaneli ya televisheni ya Al-Mayadeen ya Lebanon.
Kwa upande wake, Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran amesema: "matarajio yetu ni kuona Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki unazingatia taaluma na utaalamu na kujiepusha na kufanya mambo kisiasa".
Katika mahojiano hayo na Al-Mayadeen, Meja Jenerali Mohammad Baqeri, Mkuu wa Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, yeye ameuzungumzia mpango wa Rais Donald Trump wa Marekani kuhusu Ukanda wa Ghaza akiutaja kuwa ni "matamshi ya kijazba" tu ambayo "hayana uwezo wa kutekelezwa, na kwamba hilo litathibitishwa na wananchi wa Palestina".
Meja Jenerali Sayyid Abdolrahim Mousavi, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, yeye amezungumzia matamshi ya Trump ya eti kutaka kufanya mazungumzo na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na akasema: "hakuna mtu mwenye akili timamu anayeweza kukubali mazungumzo chini ya mashinikizo na vikwazo."
Naye Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Hassan Rouhani amesema, Wamarekani hawajawahi kupata mafanikio yoyote katika kukabiliana na Iran katika masuala ya kisiasa na kimataifa.../
342/
Your Comment