12 Machi 2025 - 18:23
Source: Parstoday
Pezeshkian: Bora tufe kwa heshima, lakini hatutaishi kwa udhalili

Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian amekosoa vikali mwenendo wa kimaksi wa utawala wa Donald Trump dhidi ya Iran na kueleza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu sio Ukraine, na katu haitafanya mazungumzo na Marekani katika mazingira ya vitisho au kulazimishwa.

"Lazima tudumishe uhusiano na ulimwengu. Hatutaki kutengwa au kugombana na mtu yeyote, lakini hiyo haimaanishi kwamba tutainama kwa udhalili mbele ya mtu yeyote," Pezeshkian amesema hayo wakati wa mkutano wa Jukwaa la Wajasiriamali wa Iran hapa mjini Tehran jana Jumanne.

Rais wa Iran amesisitiza kuwa, "Tunaweza kufa kwa heshima, lakini hatutaishi kwa aibu." Pezeshkian amepinga vikali kile alichokitaja kama makataa ya mwisho kutoka kwa Donald Trump, akirejelea barua iliyoripotiwa kutumwa na Rais wa Marekani kwa Iran.

Barua hiyo, inadaiwa, iliitaka Tehran kusitisha mipango yake ya nyuklia na makombora na kuchukua hatua nyingine mkabala wa kuondolewa vikwazo.

"Haikubaliki kwa mtu kuja na kusema, 'Usifanye hivi, usifanye vile, au vinginevyo...., sitakuja kujadiliana nawe. Nenda ukafanye chochote unachotaka," Pezeshkian amesema.

Pezeshkian: Bora tufe kwa heshima, lakini hatutaishi kwa udhalili

Hali kadhalika amemkosoa Trump kwa kutomheshimu mwenzake wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, huku akimshinikiza afikie makubaliano na Russia.

Hivi karibuni pia, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi alisema katu Jamhuri ya Kiislamu haitafanya mazungumzo kuhusu mradi wake wa nishati ya nyuklia chini ya mashinikizo, kwani mazungumzo ni tofauti na utumiaji wa mabavu na vitisho.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha