Helyeh Doutaghi, ambaye anahudumu kama Naibu Mkurugenzi wa Masuala ya Sheria na Uchumi wa Kisiasa (LPE) kwenye Chuo Kikuu cha Yale huko Marekani, ametoa taarifa ya kulaani kusimamishwa kazi na kusema kuwa kitendo hicho kimefanyika ili kulipiza kisasi dhidi ya msimamo wake wa kuunga mkono Palestina na amepinga kukanyagwa haki zake za kikatiba za uhuru wa kujieleza na wa masomo.
Katika sehemu moja ya taarifa yake, Dk Doutaghi amesema: "Akili Mnemba inatumiwa kama silaha kuwalenga wanafunzi, kitivo na waandaaji wanaothubutu kulalamikia mauaji ya umati, kuwatesa Wapalestina kwa njaa na kuangamizwa kizazi chao kunakofanywa na Israel.
Dk Doutaghi ambaye pia ni mtaalamu wa sheria za kimataifa na ni Mhadhiri Mshiriki wa Utafiti katika Chuo cha Sheria cha Yale, amearifiwa kwamba kilichomponza ni makala yake ya Machi 3, 2025 iliyokosoa vikali jinai za Israel huko Palestina. Tovuti ya Jewish Onliner imemwita kuwa ni gaidi.
Doutaghi amekuwa akipaza sauti kubwa kuhusiana na athari za operesheni za kijeshi za Marekani, ubeberu na mauaji ya umati ya Marekani na Wazayuni na mgogoro wa kibinadamu unaoendelea huko Palestina. Analalamika kwamba makala zake zinamfanya akumbwe na unyanyasaji mtandaoni na hata vitisho vya kuuawa.
342/
Your Comment