Mjumbe huyo wa Marekani amekariri madai ya Washington na kusema: Rais Donald Trump ameeleza wazi kwamba miradi ya nyuklia ya Iran ni tishio kwa amani na usalama wa kimataifa na kwamba Baraza la Usalama lina jukumu la kuulinda.
Mjumbe wa Marekani katika Umoja wa Mataifa amedai kuwa: Kama alivyoripoti Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA), Tehran inaendelea kuzalisha kwa kasi urani iliyorutubishwa kwa kiwango cha juu.
Mjumbe huyo wa Marekani ameendelea kudai kuwa: Iran inaendelea kulikaidi waziwazi Baraza la Usalama, kukiuka wajibu wake kuhusu masuala ya usalama ya IAEA, na kupuuza wasiwasi wa wazi na thabiti wa Baraza la Usalama na jamii ya kimataifa.
Huko nyuma, James Kariuki Balozi na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Uingereza katika Umoja wa Mataifa alitoa kauli za chuki na kudai kuwa kila aina ya hatua za kisiasa zitatumika dhidi ya Iran ili kuizuia kumiliki silaha za nyuklia.
Wakati huo huo, Fu Cong Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa amesema anataraji kuwa pande zote katika faili la nyuklia la Iran zitashirikiana ili kupata suluhu ya suala hili.
342/
Your Comment