Hujjatul Islam Sayyid Mohammad Hassan Abu Torabi Fard amesema hayo katika hotuba za Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran (Machi 14), katika ukumbi wa Muswalla Imam Khomeini (RA). Ameongeza kuwa: "Hii leo mnashuhudia waziwazi vitisho vya viongozi wa Marekani na wakati huo huo wanaaomba kufanya mazungumzo na Iran; hii ni mienendo miwili inayokinzana."
Hatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran amesisitiza kuwa: "Ulimwengu wa Kiislamu unasimama kwa umoja na mshikamano dhidi ya sera za kupenda kujitanua na za kibeberu na hautalegeza kamba kwenye misimamo yake ya haki."
Hujjatul-Islam Abu Turabi Fard amesema: Leo Iraq, Palestina, na mashujaa wa Yemen ni nembo ya izza na misimamo hiyo ya kupambana na makafiri, na Lebanon ni nembo ya Muqawama dhidi ya madhalimu.
Akizungumzia mazoezi ya pamoja yaliyoshirikisha majeshi ya majini ya nchi tatu za Iran, Russia na China, katika maji ya eneo la Iran kaskazini mwa Bahari ya Hindi yaliyopewa jina la Mkanda wa Usalama 2025 (Security Belt-2025), hatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran amesema kuwa, lengo la maneva hayo makubwa ni kudhihirisha uwezo wa jeshi la Iran kwa ushirikiano na nchi nyingine.
Hatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran, amechambua Aya ya 54 ya Suratu Al-Maidah na kusema: “Mwenyezi Mungu hawapendi wafujaji, na katika hali ya sasa ya upunguufu wa maji, wananchi wanapaswa kuweka kipaumbele katika kurekebisha utaratibu wa matumizi yao na kupunguza kiasi cha maji yanayotumika majumbani.
342/
Your Comment