Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (A.S) - Abna -: Sayyid Abdul Malik Badr al-Din al-Houthi, Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah jana Jumapili alitoa hotuba kuhusu hujuma ya Marekani dhidi ya nchi hii na kusema kuwa Marekani imeanza duru mpya ya mashambulizi dhidi ya Yemen.
Akirejelea ukweli kwamba Marekani ilishambulia kwa mabomu nyumba na maeneo ya makazi ya raia huko Sana'a na majimbo kadhaa ya Yemen, Al-Houthi ameongeza kuwa: Mashambulio haya yamesababisha makumi ya watu kuuawa shahidi wakiwemo Wanawake na Watoto.
Akieleza kuwa mashambulizi ya Marekani ni mwendelezo wa mashambulizi dhidi ya Umma wa Kiislamu, alifafanua: Lengo la Marekani liko wazi; Nalo ni kusaidia adui wa Israel.
Al-Houthi amesema: Uchokozi huo wa Marekani ulitekelezwa baada ya sisi kutangaza msimamo wetu wa wazi kuhusu kuwaunga mkono Wananchi wa Palestina dhidi ya siasa za utawala haram wa Kizayuni za kuwaua kwa njaa watu wa Ghaza.
Katibu Mkuu wa Ansarullah ameashiria zaidi ukimya wa nchi za eneo hili (la kikanda la Mashariki ya Kati) kuhusiana na jinai zinazofanywa na Wazayuni wa Ghaza na kusema: Kwa bahati mbaya, misimamo ya nchi za Kiislamu na Kiarabu kuhusu suala hili imekuwa baridi sana. Hakuna hatua za dhati zilizochukuliwa ili kumzuia adui Mzayuni kuwasababishia njaa watu wa Gaza.
Al-Houthi ameongeza kuwa: Sasa hivi adui Mzayuni anajaribu kujenga kiu huko Ghaza na kuizuia Ghaza isiwafikie watu wake. Suala la kuwabakisha kwa njaa watu wa Ghaza na kuzuia misaada ya chakula isiweze kuwafikia ni kitendo cha kuelekea kwenye mauaji ya watu hao.
Katibu Mkuu wa Mapinduzi ya Yemen ameongeza kuwa: Wakati adui Mzayuni kwa ushirikiano wa Marekani anapofanya mauaji ya kimbari huko Ghaza, huu unakuwa ni mstari mwekundu kwetu sisi ambapo hatuwezi (kuishia) kuwa watazamaji mbele yake.
Alisema kuwa "wakati adui Mzayuni anapoelekea kwenye mauaji ya halaiki huko Gaza kwa ushiriki wa Marekani, huu unakuwa ni mstari mwekundu kwetu sisi na hatuwezi kusimama tu bila kufanya lolote (na kuishia) kuwa watazamaji mbele yake," na kuongeza: Kuhusu suala hili, kuna faradhi za kisheria na kiutu hata kwa wasio Waislamu, lakini kila mtu katika jamii ya ulimwengu anashindwa kutekeleza wajibu wake, lakini kwa jinsi alivyoeleza Mtume wa Uislamu (rehema na amani ziwe juu yake na Aali zake), sisi ni Umma mmoja.
Al-Houthi amesema: Uamuzi wa Yemen wa kuunga mkono Watu wa Palestina ni sehemu ya ahadi za kibinadamu na kidini na shinikizo la misaada ya kibinadamu kuingia Ghaza na kumaliza njaa ya Wapalestina milioni 2.
Ameongeza kuwa: Kinachotokea Ghaza si suala la kawaida ambalo linaweza kupuuzwa au kupitishwa tu (kwamba liache lipite), bali ni suala zito na ni jinai kubwa dhidi ya sehemu kubwa ya Wananchi wa Palestina.
Sayyid Abdul Malik Badr al-Din al-Houthi ameeleza masikitiko yake kwamba tawala za ulimwengu wa Kiislamu hususan katika ulimwengu wa Kiarabu zina misimamo dhaifu dhidi ya Ghaza na kusema: Kwa sababu hakuna hatua yoyote ya dhati inayochukuliwa na tawala hizo ili kuzuia siasa za adui Mzayuni za kuleta njaa dhidi ya watu wa Ghaza, ambayo hivi sasa imefikia mahali ambapo inataka kuwanyima maji na kuwafanya wawe na kiu.
Akiashiria kwamba Wamarekani na Waisraeli wana malengo makubwa na miradi ya jinai na kichokozi inayoulenga Umma wa Kiislamu, ameongeza kuwa: Wamarekani na Waisraeli wana misingi ya kiitikadi, mielekeo ya kikoloni na mienendo ya ukatili na jinai.
Katika hotuba yake, al-Houthi ametoa wito kwa watu wa nchi hii (Yemen) kujitokeza kwa wingi na kwa shauku katika maandamano makubwa ya kesho, yatakayofanyika kwa mnasaba wa kumbukumbu ya Vita vya Badr.
Ametangaza kwamba wakati halisi wa maandamano haya na hatua zingine zinazohusiana nayo zitaamuliwa na kamati za maandalizi.
Akizungumzia umuhimu wa maandamano haya, al-Houthi amesisitiza kuwa uwepo mkubwa wa watu unaonyesha kushikamana kwao na maadili ya Kiislamu na misimamo ya upinzani (Muqawamah) dhidi ya ukandamizaji na udhalimu.
Akaongeza kusema: Msimamo wetu ni kuendelea kwa Njia ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) na Bendera ya Uislamu, na tutashikamana na misimamo ya Kiislamu na Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu katika zama hizi.
Katibu Mkuu wa Ansarullah Yemen amewataka Wananchi kushiriki katika matembezi hayo kwa imani, uaminifu na azma na kulifanya tukio hili kuwa ishara ya subira na ustahimilivu wao mbele ya changamoto.
Akiwahutubia watu wa Yemen alisema: Katikati ya Bahari hii ya udhaifu na kusalimu amri, nyinyi ni mwendelezo wa Njia ya Uislamu sahihi na mmepandisha juu Bendera ya Uislamu ili (kutambua na) kuitimiza nafasi sahihi ya haki anayoitaka Mwenyezi Mungu.
Akiwahakikishia watu wa Yemen, al-Houthi alitangaza kuwa hali ya nchi hiyo ni imara na shwari kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu na uzoefu uliopatikana katika miaka ya Upinzani (Muqawamah).
Alikazia zaidi kwa kusema: Tunamtegemea Mwenyezi Mungu kabisa na kutumaini msaada Wake. Mabadiliko yoyote yatatokea, kwa msaada wa Mwenyezi Mungu na uzoefu wetu katika kukabiliana na maadui, hali yetu itabaki kuwa imara na thabiti.
Your Comment