17 Machi 2025 - 18:25
Source: Parstoday
Rais wa China akataa mwaliko wa EU wa kuhudhuria kikao cha kuadhimisha miaka 50 ya uhusiano

Rais Xi Jinping wa China amekataa mwaliko wa kuhudhuria kikao kilichopangwa kufanyika mjini Brussels kuadhimisha miaka 50 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi yake na Umoja wa Ulaya.

Hivi karibuni China ilikosoa vikali taarifa iliyotolewa na baadhi ya nchi za Ulaya zinazounda kundi la G7 kuhusiana na Taiwan.

Baadhi ya wachambuzi wanaitakidi kuwa msimamo wa Rais Xi wa China wa kukataa mwaliko wa Ulaya unahusiana na kutofurahishwa Beijing na taarifa hiyo iliyotolewa na nchi wanachama wa EU.

Ubalozi wa China mjini Ottawa, Canada mahali kilipofanyika kikao cha nchi wanachama wa G7 umejibu taarifa ya pamoja ya mawaziri wa mambo ya nje wa kundi hilo ukisema: "eneo la Asia-Pasifiki ni uga wa kuleta amani na maendeleo, si ubao wa shataranji ya mashindano yenu ya kijiopolitiki".

Beijing imesisitiza pia kwamba, Taiwan ni sehemu isiyoweza kutenganishwa na ardhi ya bara ya China na kwamba suala la kisiwa hicho ni kadhia ya ndani tu ya Beijing, na ufunguo wa kudumisha amani na utulivu katika Mlango-Bahari wa Taiwan ni kufungamana na "Kanuni ya China Moja" na kuwapinga kikamilifu wanaotaka kujitenga Taiwan; na kwa hiyo ushiriki wowote wa kisiwa hicho katika mashirika ya kimataifa lazima uendane na "Kanuni ya China Moja".

Taarifa hiyo ya ubalozi wa China mjini Ottawa imeongeza kuwa, Beijing inatetea kwa uthabiti mamlaka yake ya utawala ya eneo lake la ardhi, haki zake na maslahi yake ya baharini na inalaani hatua zenye madhara za G7 dhidi ya mamlaka ya utawala ya China.

Kundi la G7, linalojumuisha Ufaransa, Ujerumani, Italia, Uingereza, Marekani, Canada na Japan, limeunga mkono kushiriki Taiwan katika mashirika na taasisi za kimataifa katika mkutano wao wa hivi karibuni uliofanyika nchini Canada.../

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha