Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (a.s) - Abna - Katika mkutano wa mapitio ya mfululizo wa TV wa filamu ya "Muawiyah", wataalam walikaa na kupitia mfululizo huu (na kuuchambua).
Mfululizo wa - filamu ya - “Muawiya” ni kinyume na - maoni na - nadharia ya Sunni
Dk. Mehdi Farmanian, Profesa wa Chuo Kikuu cha Dini na Madhehebu, alisema katika mkutano huu: Leo, Mawahabi wanakusudia kuitambulisha fikra ya Uthmaniyya kuwa ni fikra (maalum) ya Sunni kwa kutumia mfululizo wa - filamu ya – Muawiyah; hali ya kuwa hayo ni mawazo (na fikra ya) ya Ibn Taymiyyah, na Masunni wanapinga (kabisa) na fikra hizo.
Akaongeza: Wanachuoni wetu na wakubwa wetu kidini wasikamilishe fumbo la adui; Kwa sababu Mawahabi wanajaribu kuanzisha vita kati ya Shia na Sunni; Wakati tofauti kubwa iliyopo ni baina ya Masunni na Mawahabi. Kwa hiyo, inawezekana kukabiliana na mfululizo huu (wa filamu ya Muawiya) kwa kuakisi ukosoaji wa Wanachuoni (Maulamaa) wa Kisunni.
Profesa huyu wa Chuo Kikuu alisema: Mfululizo huu umejaribu kuzingatia historia ya Ahlu - Sunna, lakini pia kutekeleza amri za mwajiri wake wa Kiwahabi. Kwa hiyo, wanahistoria wanaweza kuukosoa mfululizo huu kwa kuashiria matatizo mengi ya kihistoria ya mfululizo huu kwa mujibu wa vyanzo vya Sunni (Ahlu - Sunna).
Mfululizo wa Mu'awiyah sio maoni (nadharia) ya Sunni
Dk. Essam Yahya Al-Emad, Mtafiti wa Sayansi ya Kiislamu na Mwanafikra wa Yemen, alisema kuhusu mtazamo wa Wanazuoni (Maulamaa) wa Kisunni kuhusu Muawiyah: Hassan al-Banna alikuwa dhidi ya Muawiyah, Ahmad Sediq Ammari aliandika kitabu dhidi ya Muawiyah, na hata Ibn Jauzi, ambaye alikuwa Msalafi, aliandika athari (Kitabu) katika kumkataa (na kumradi) Yazid.
Waundaji wa mfululizo wa Muawiyah hawakubali imani (itikadi) za Sunni na Shia. Kwa hiyo, haiwezi kusemwa kwamba mfululizo wa Muawiyah ni matokeo ya tofauti kati ya Iran na Saudi Arabia, na kwa upande mwingine, mifululizo ya - filamu ya - Iran inazingatia mtazamo wa Sunni.
Mtafiti huyu wa Sayansi ya Kiislamu alisema: Ni dhulma kuanzisha mfululizo wa Muawiyah kwa anuani ya mtazamo wa Sunni. Waundaji wa mfululizo wa Muawiyah wameegemezwa kwenye mtazamo wa wale walioitilia shaka historia ya (Mwanachuoni mkubwa wa Historia wa Kisunni, aitwaye) Tabari kuwa kama marejeo ya historia ya Sunni.
Tarikh al-Tabari ni Kitabu ambacho kinatumiwa sio tu na Masunni (pekee), bali pia na Mashia. Waumbaji (watengenezaji wa mfululizo) wa Muawiyah hawakutumia vitabu vya “Tarikh al-Tabari” na historia ya Ibn Kathir kwa sababu nadharia waliyowasilisha kuhusu Muawiyah katika mfululizo huu ni kinyume na vitabu hivi.
Mwanachuoni huyu wa sayansi ya Kiislamu alisema: Kwa hiyo, mfululizo wa Muawiyah ni kinyume na historia ya Tabari, kwa sababu historia iliyotajwa na Muawiyah katika vyanzo vya kihistoria vya Kisunni haitofautiani na historia mbele ya Mashia.
Mwanachuoni huyu wa sayansi ya Kiislamu alisema: Kwa hiyo, mfululizo wa Muawiyah ni kinyume na Kitabu cha Historia cha Tabari (Tarikh Al-Tabari), kwa sababu historia iliyotajwa kuhusu Muawiyah katika vyanzo vya kihistoria vya Kisunni haitofautiani na historia (yake namna ilivyotajwa) kwa Mashia.
Mfululizo wa Dola Milioni 100!
Hojjatul Islam "Mortaza Falah", mtaalamu wa vyombo vya habari na mkosoaji wa filamu, alisema:
Mfululizo wa Muawiyah ulitayarishwa na kampuni ya MBC, mfululizo huu ulipaswa kuonyeshwa miaka miwili iliyopita, lakini uliahirishwa kutokana na vipingamizi. Bajeti ya mfululizo huu ni Dola milioni 100.
Katika miaka ya hivi karibuni, nchi za Kiarabu zimeingia katika uzalishaji wa mifululizo (ya filamu) ya kimkakati, na mwaka huu, kwa mujibu wa sera zilizofuatwa na baadhi ya nchi za Kiarabu, mfululizo wa Muawiya umetolewa. Lakini jumuiya ya Sunni haikubaliani kabisa na uwasilishaji wa sura (taswira) hii ya Muawiyah.
Akaongeza: Moja ya matatizo ya mfululizo huo ni kwamba shakhsia za wahusika hazijasawiriwa (kwa ibara nyingine: Taswira zao hazijawekwa katika sura sahihi) ipasavyo, kwa mfano, Muawiyah (kihistoria) alikuwa ni mtu mnene ambaye alikuwa akila sana (alikuwa 'Mlafi', na Mlafi maana yake ni Mtu anayependa kula sana), na Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake na Aali zake) alimlaani kuwa atakuwa anakula sana lakini bila kushiba (hii ni laana ya Mtume s.a.w.w kwa Muawiyah), lakini katika mfululizo wa filamu ya Muawiyah, tunaona kwamba Muawiyah anasawiriwa (anapewa taswira ya) kuwa ni shakhsia aliyejengeka vizuri. Kwa mfano, kusilimu kwa Muawiyah kabla ya kutekwa kwa Makka (kabla ya Ushindi wa Makka) ni mojawapo ya sehemu za upotoshaji.
Aina nyingine ya tatizo la maudhui ni kushindwa kusimulia matukio muhimu ya kihistoria ili waweze kuendeleza lengo lao kuu, ambalo ni kumtakasa Muawiyah na Bani Umayyah.
Uso halisi wa Muawiyah umefichwa kwenye mfululizo
Hojjatul Islam Adriani, Mtaalamu wa filamu, alisema: Mfululizo huu unalenga kutakasa uso wa watu kama vile Abu Sufyan. Mfululizo huu wa Muawiyah ulimtambulisha Abu Sufyan kama mwangalizi wa vita vya Uhud, na sio mtu (aliyekabiliana au) aliyesimama mbele (dhidi) ya Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Mtaalamu huyu wa vyombo vya habari alisema: Hadhira (wanaolengwa kufikishiwa fikra) ya mfululizo huu ni mashahidi wa utakaso wa Muawiyah; Kama vile al-Julani huko Syria alivyoficha hali yake ya ugaidi nyuma ya suti yake, mfululizo huu pia unajaribu kuficha (tabia au) shakhsia halisi ya Muawiyah.
Your Comment