20 Machi 2025 - 17:37
Source: Parstoday
San'a: Iran haiingilii hata chembe maamuzi ya Yemen

Waziri wa Mambo ya Nje wa Yemen amesisitiza kuwa: Iran haingilii hata chembe maamuzi ya serikali ya San’a na kwamba operesheni za Yemen dhidi ya Wazayuni ni uamuzi huru na utaendelea kutekelezwa kivitendo hadi mzingiro wa Ghaza utakapovunjwa kikamilifu.

Shirika la Habari la Tasnim limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, wakati Yemen inashikilia msimamo wake wa kuiunga mkono Ghaza na kuendelea kuzuia vyombo vya majini vya Israel visitumie Bahari Nyekundu, bila ya kujali vitisho, uchokozi na mashinikizo yoyote ya Marekani, Uingereza na Wazayuni wengine, Waziri wa Mambo ya Nje wa Yemen Jamal Amer amebainisha wazi kuwa, Jeshi la nchi yake halitopunguza wala kusimamisha operesheni zake dhidi ya meli za Israel katika Bahari Nyekundu mpaka utawala wa Kizayuni utakapokomesha jinai zake dhidi ya Wapalestina wa Ghaza.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Yemen amesema hayo katika mahojiano na shirika la habari la Reuters na huku akijibu madai ya Marekani kwamba Iran inaathiri maamuzi ya Yemen amesema kwamba, hakutakuwa na mazungumzo ya kupunguza operesheni za Yemen dhidi ya utawala wa Kizayuni. Kitu pekee kitakachopunguza mashinikizo hayo ni kuacha Israel kuizingira Ghaza. Iran haingilii hata cbhembe maamuzi ya Yemen. Baadhi ya wakati Tehran inapatanisha baadhi ya masuala, lakini haitwishi misimamo na mapendekezo yake. Yemen yenyewe ndiyo yenye maamuzi ya mwisho kuhusu mambo yake.

Katika sehemu nyingine ya mahojiano hayo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Yemen amesema: "Kuna ujumbe kutoka kwa baadhi ya madola wa kututaka tupunguze mashinikizo yetu kwa Israel, lakini hivi sasa Yemen iko katika hali ya vita na Marekani, jambo ambalo lina maana kwamba tuna haki ya kujihami kwa njia zote zinazowezekana hata kama kujihami kwetu kutapelekea kuongezeka mivutano.”

Amesema: "Tutajibu mashambulizi ya Marekani kutokea sehemu yanapofanyika. Kwa mfano, ikiwa Wamarekani watashambulia Yemen kutoka kwenye manuwari yake ya kubeba ndege ya Harry S. Truman, nasi tutaiiga manuwari hiyo."

Kuhusiana na nafasi ya nchi za Kiarabu katika uvamizi wa Marekani dhidi ya Yemen, Waziri wa Mambo ya Nje wa Yemen amesema kuwa, Saudi Arabia au nchi nyingine za Kiarabu bado hazijaingilia kijeshi katika suala hilo, na Wayemen wanapongeza msimamo huo, lakini tunazionya nchi za Kiarabu kwamba iwapo zitatumbukia katika mtego wa Marekani wa kuingilia kijeshi Yemen, nazo zote zitakuwa ndani ya shabaha za majibu yetu ya kijeshi. 

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha