Iravani, amekanusha shutuma hizo zisizo na msingi katika barua yake kwa Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kwa Katibu Mkuu wa umoja huo, iliyozungumzia shutuma zilizotolewa na Marekani na Israel dhidi ya Tehran katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na akabainisha kwa kusema: "shutuma hizi si chochote zaidi ya jaribio linalofanywa kwa mahesabu kamili ili kupotosha maoni ya umma kimataifa kwa kuyaondoa kwenye vita vya mauaji ya kimbari, jinai za kivita na ukatili mkubwa unaofanywa na utawala wa Israel dhidi ya watu wa Palestina huko Ghaza".
Mwanadiplomasia huyo mwandamizi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa: "tuhuma hizo zisizo na msingi kwa mara nyingine tena zinazidi kudhihirisha sera za uadui za serikali ya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na zinathibitisha kwamba ofisi ya uwakilishi wa kudumu wa Marekani katika Umoja wa Mataifa chini ya muongozo wa moja kwa moja wa Washington inapuuza ukweli wa mambo na inaendelea kila mara kutoa tuhuma zisizo na msingi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran."
Iravani amebainisha kuwa: katika kila fursa inayopata, ofisi ya uwakilishi wa kudumu wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, inaligeuza Baraza la Usalama kuwa chombo cha kuendelezea ajenda ya kisiasa ya Washington na kutoa taswira isiyo sahihi, ya Iran kuwa tishio kwa amani na usalama wa kimataifa.
Sehemu moja ya barua hiyo kwa Rais wa Baraza la Usalama Cristina Fernandez de Kirchner na kwa Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres imesema, tuhuma dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zinalenga kuficha ushirika usiokanushika wa Marekani katika jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Ghaza na uungaji mkono wake wa dhati kwa vitendo vya uharibifu na uvunjifu wa amani vya utawala huo katika eneo zima la Asia Magharibi.
Kwa kujibu madai yasiyo na msingi yaliyotolewa na mwakilishi wa Marekani kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran barua ya Iravani imesisitiza kuwa shughuli za nyuklia za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni za amani kabisa na zinatekelezwa kikamilifu ndani ya fremu ya majukumu ya Iran chini ya Mkataba wa Kuzuia Uenezaji wa Silaha za Nyuklia.../
342/
Your Comment