Wizara ya Mambo ya Nje ya China imetangaza katika taarifa iliyotoa siku ya Ijumaa kwamba, Marekani inapaswa iache kuingilia ushirikiano wa kibiashara kati ya China na Iran.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari, Mao Ning, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China amesema: "Marekani inapaswa iache kuingilia ushirikiano wa kibiashara na kiuchumi kati ya China na Iran".
Msemaji huyo wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China ameongezea kwa kusema: "Beijing itachukua hatua zote zinazohitajika kwa ajili ya kulinda kwa uthabiti haki za kisheria na maslahi halali ya makampuni ya China".
Hayo yanajiri baada ya Wizara ya Fedha ya Marekani kutangaza kuwa imewawekea vikwazo vipya baadhi ya watu, taasisi na meli kadhaa za Iran.
Pasi na kuashiria namna viongozi wenyewe wa Marekani walivyokiri kuhusu kufeli kwa kampeni ya vikwazo vya juu kabisa dhidi ya Iran iliyotekelezwa katika muhula wa kwanza wa urais wa Trump, wizara ya fedha ya nchi hiyo ilitangaza siku ya Alkhamisi kwamba, "Marekani imetekeleza awamu ya nne ya vikwazo dhidi ya Tehran, kwa kuzingatia Hati ya Usalama wa Taifa ya Rais na kampeni ya mashinikizo ya juu kabisa ya Rais Trump dhidi ya Iran, ili kulenga mauzo ya mafuta ya Iran".
Kama ilivyoelezwa katika taarifa ya wizara ya fedha ya Marekani, siku ya Alkhamisi Washington iliongeza "raia mmoja wa China, makampuni 13, na makampuni manane yenye uhusiano na Iran" katika orodha ya vikwazo dhidi ya Tehran.
Taarifa hiyo ilidai kuwa akthari ya makampuni yaliyowekewa vikwazo yako nchini China. Aidha, meli zilizowekewa vikwazo ni zile zinazopeperusha bendera za nchi tofauti zikiwemo za Panama, Comoro na Barbados.../
342/
Your Comment