Carney amebainisha kuwa Rais wa Marekani Donald Trump hatimaye ataheshimu mamlaka ya Canada na kuwa tayari kwa mazungumzo ya kina ya kibiashara kwa sababu Wamarekani wataumizwa na vita vya kibiashara vya Trump.
Waziri Mkuu wa Canada alitangaza siku ya Ijumaa kwamba, mazungumzo na Trump hayatafanyika "mpaka tupate heshima tunayostahili kama taifa huru. Na haya si matarajio makubwa".Trump aliendeleza mashambulizi yake ya kila siku dhidi ya Canada siku ya Ijumaa aliporudia kauli yake kwamba nchi hiyo inapasa iwe jimbo la 51 la Marekani na kwamba Marekani inaifanya Canada "iendelee."
"Ninaposema wanapaswa wawe ni jimbo, ninakusudia hivyo kwa dhati," alisisitiza rais huyo wa Marekani.Kwa upande wake, Waziri Mkuu mpya wa Canada amesema anataka majadiliano ya kina kuhusu biashara na usalama na Wamarekani na si mazungumzo ya mara moja tu ya ushuru.
Carney amesisitiza kwa kusema: "mwishowe, Wamarekani watashindwa kutokana na hatua ya kibiashara ya Marekani, na hiyo ndiyo sababu mojawapo inayonifanya niamini kwamba kutakuwa na mjadala huo utakaofanyika kwa heshima na upana ufaao" na akaongezea kwa kusema: "niko tayari kwa hilo wakati wowote wakiwa tayari".
Kauli za kila siku anazotoa Trump dhidi ya uhuru wa Canada zimewakasirisha Wacanada, ambao wanaghairi kufanya safari za kuelekea Marekani na kuepuka kununua bidhaa za nchi hiyo kadiri wawezavyo.Hayo yanajiri wakati Canada inatarajiwa kuzindua kampeni ya matangazo leo Ijumaa katika majimbo 12 ya Marekani ili kukabiliana na ushuru wa nchi hiyo.. Hayo ni kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje Melanie Joly.
Katika mahojiano na CNN, Joly amesema: "tunazindua kampeni ya matangazo leo katika majimbo 12 tofauti. Wacanada wanatuma ujumbe kwamba hakuna mshindi katika vita vya kibiashara. Kutakuwepo na ukosefu wa ajira katika pande zote mbili za mpaka".../
342/
Your Comment