22 Machi 2025 - 21:32
Source: Parstoday
Google kutumia majasusi wa Israel waliohusika na mauaji ya kimbari ya Gaza

Kampuni ya Google mapema wiki hii ililipa dola bilioni 32 ili kununua kampuni ya Israel ya usalama wa mtandao, Wiz, ambayo inaendeshwa na wafanyakazi wa zamani wa Unit 8200, kitengo maalumu cha upelelezi wa mtandao cha jeshi la Israel.

Ununuzi huo unaashiria uhamisho mkubwa zaidi wa majasusi wa Israel kwenda katika kampuni ya Marekani.

Unit 8200 ya Israel ni timu ya siri ya vita vya mtandaoni ambayo inasemekana kujenga mfumo wa akili mnemba (AI) ambao uliusaidia utawala huo katili kufanya mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Palestina katika Ukanda wa Gaza.

Unit 8200 ilitayarisha programu na kuunda algoriti ambazo zilisimamia mauaji ya kimbari ya watu wa Gaza, na pia ilihusika na shambulio la vifaa vya pager huko Lebanon. Sasa wanaume na wanawake waliosaidia kubuni utawala wa ubaguzi wa rangi wamemezwa na kampuni kubwa ya teknolojia ya Marekani.

Makundi ya utetezi yanasema, akili mnemba (AI) na kujifunza kwa mashine ndio msingi wa usanifu wa uvamizi na ubaguzi wa rangi ulioanzishwa kabla ya kampeni ya mauaji ya kimbari ya Gaza, kutokana na matumizi ya teknolojia ya utambuzi wa uso, na bunduki zinazoelekezwa na AI kwenye vituo vya ukaguzi, hadi kwenye programu za ujasusi za Israel zinazojulikana kama 'Blue Wolf' na 'Red Wolf'.

Makubaliano ya Google na Wiz yanawakilisha mapinduzi makubwa ya kikodi kwa utawala wa haramu wa Israel. Makubaliano hayo yataingiza karibu dola bilioni 5 ya mapato kwa uchumi wa vita, au karibu 0.6% ya Pato la Taifa la utawala bandia wa Israel.

Kampuni ya Google imewekeza sana Israel. Ilifungua ofisi huko karibu miaka 20 iliyopita, imenunua idadi ya makampuni ya teknolojia ya Israel katika miaka ya hivi karibuni, na Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa kampuni hiyo, Eric Schmidt ametangaza uaminifu wake kwa nduli Benjamin Netanyahu mara nyingi katika miaka ya karibuni.

Google kutumia majasusi wa Israel waliohusika na mauaji ya kimbari ya Gaza

Maafisa wote muhimu na wakuu katika kampuni ya Google na kampuni mama, Alfabet, ni watu wanaojifakharisha kuwa Wazayuni.

Hivi sasa ambapo uchumi wa Israel unayumba, watu  wengi wakikimbilia nje ya Israel, jeshi lake haliwezi kushinda vita huko Gaza na Netanyahu akikabiliwa na matatizo makubwa, biashara ya Google na wa Wiz inaupa utawala huo katili msukomo unaohitajika sana.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha