Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (AS) - Abna -; Katika sehemu zilizotangulia za makala hii, (Sehemu ya 1, Sehemu ya 2) nafasi ya Uimamu katika Dua ya kabla alfajiri (muda wa daku) katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ilichunguzwa na Maimamu wa Kizazi cha Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w) waliletwa kama mifano kamili ya baadhi ya masuala yaliyotolewa katika Dua hii. Katika makala hii, sehemu nyingine za Dua hii yenye mwanga na uhusiano wake na Maimamu Maasumin (AS) zimechambuliwa.
اللّٰهُمَّ إِنِّی أَسْأَلُکَ مِنْ کَلِماتِکَ بِأَتَمِّها وَکُلُّ کَلِماتِکَ تامَّةٌ، اللّٰهُمَّ إِنِّی أَسْأَلُکَ بِکَلِماتِکَ کُلِّها
Istilahi ya “Neno” ina maana pana, kwa mfano “Maji” ni neno, yaani ni jina na ishara ya kuashiria, kutambulisha na kutambua kitu. Katika Aya mbalimbali za Qur'an Tukufu, neno "Neno la Mwenyezi Mungu / كلمة الله" pia limetumika. Kwa mfano, katika Surah al-Tawba, Aya ya 40, inasema:
«جَعَلَ کَلِمَةَ الَّذِینَ کَفَرُواْ السُّفْلَی وَکَلِمَةُ اللّهِ هِیَ الْعُلْیَا وَاللّهُ عَزِیزٌ حَکِیمٌ».
Aya hii inazungumzia maneno ya wale waliokufuru, na "Neno la Mwenyezi Mungu" ndilo lililotukuka.
Pia, katika Surah Al-Imran, Aya ya 45, inayozungumzia kuzaliwa kwa Yesu (a.s), imeelezwa:
«إِنَّ اللّهَ یُبَشِّرُکِ بِکَلِمَةٍ مِّنْهُ اسْمُهُ الْمَسِیحُ».
Mwenyezi Mungu anakubashiria kwa "Neno" kutoka Kwake, ambaye jina lake ni Masih (Isa bin Maryamu).
Pia, katika Surah Baqarah, Aya ya 37, kuhusu suala la Toba ya Nabii Adamu (a.s), Mwenyezi Mungu alisema:
«فَتَلَقَّی آدَمُ مِن رَّبِّهِ کَلِمَاتٍ فَتَابَ عَلَیْهِ».
"Kisha Adam akapokea "Maneno" kutoka kwa Mola wake na Mwenyezi Mungu akamkubalia Toba yake.
Imeelezwa pia katika Surah al-Kahf, Aya ya 109:
«قُلْ لَوْ کانَ الْبَحْرُ مِداداً لِکَلِماتِ رَبِّی لَنَفِدَ الْبَحْرُ قَبْلَ اَنْ تَنْفَدَ کَلِماتُ رَبِّی».
"Sema: Lau Bahari ingelikuwa wino wa kuandika "Maneno" ya Mola wangu Mlezi, basi Bahari itamalizika kabla ya kumalizika "Maneno" ya Mola wangu Mlezi.
Katika Surah Luqman, Aya ya 27, pia kuna maelezo haya kuhusu "Maneno ya Mwenyezi Mungu":
«وَ لَوْ اَنَّ ما فِی الْاَرْضِ مِنْ شَجَرَةٍ اَقْلامٌ وَ الْبَحْرُ یَمُدُّهُ مِنْ بَعْدِهِ سَبْعَةُ اَبْحُرٍ ما نَفِدَتْ کَلِماتُ اللَّهِ اِنَّ اللَّهَ عَزِیزٌ حَکِیمٌ».
"Lau yaliyomo yote ardhini katika miti yangelikuwa ni kalamu, na bahari ikachanganywa kwa ajili yake, na bahari saba zikiongezwa juu yake(zote zikawa kama wino wa kuandikia), hayo yote yatakoma na kuisha; lakini "Maneno" ya Mwenyezi Mungu hayataisha; Mwenyezi Mungu ana nguvu na hekima".
Katika Aya ya 124 ya Surah Baqarah, Aya ya 34 ya Surah An'am na Aya ya 64 ya Surah Mubarak Yunus, neno "Maneno ya Mwenyezi Mungu" pia limetajwa.
Kwa njia hii, inaweza kusemwa kwamba chochote kinachowakilisha "Udhihirisho wa Mwenyezi Mungu" kinaweza kujulikana kama “Maneno ya Mwenyezi Mungu” na miongoni mwa "Maneno" haya, bila shaka, Maimamu (a.s) wameonyesha udhihirisho mkubwa zaidi wa Mwenyezi Mungu.
Katika riwaya mbalimbali, Maimamu Maasumin (AS) wametambulishwa kama “Neno Kamili la Mwenyezi Mungu”. Yahya Ibn Aktham alimuuliza Hazrat Hadi (AS) kuhusu Aya hii: Nini maana ya “Maneno ya Mwenyezi Mungu”? Imam Hadi (a.s) alisema:
«نَحْنُ الْکَلِمَاتُ الَّتِی لَا تُدْرَکُ فَضَائِلُهَا وَ لَا تُسْتَقْصَی»(۱).
"Sisi ni Maneno ya Mungu, ambayo fadhila zake hazidirikiwi na hazikomi".
Imetajwa pia katika jumla za hadithi nariwaya kuhusu Ahlul-Bayt (a.s) kwamba walisema:
«نحن الکلمات التامّات».(۲).
Yaani: "Sisi ndio Maneno kamili na kamilifu ya Mungu".
Kwa mantiki hiyo, inaweza kusemwa kwamba: Makusudio ya "Maneno Kamili ya Mungu" katika sala ya kabla ya alfajiri katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni Maimamu Maasumina (a.s), ambao wameweza kuonyesha maonyesho naudhihirisho wa Mwenyezi Mungu kwa njia inayofaa.
Katika sehemu nyingine za uandishi huu, tutaeleza zaidi uhusiano uliopo kati ya Dua ya kabla ya alfajiri katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na Ahlul-Bayt (AS).
-
Vyanzo:
1- Bihar al-Anwar, Juzuu ya 4, ukurasa wa 151, Na kitab al-Ihtijaj: Juzuu ya 2, ukurasa wa 454. Kitab al-Ikhtiswas: Ukurasa wa 90.
2- Bihar al-Anwar, Juzuu ya 5, ukurasa wa 9.
3- Kitabu cha Sharhi ya Dua ya Kabla ya Al-Fajiri, Imam Khomeini (RA).
Sayyid Ali Asghar Hosseini / Abna.
Your Comment