Donald Tusk ametangaza kuwa: Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamefikia mapatano kuwa umoja huo unapasa hadi kufikia mwaka 2030, kuwa na uwezo kamili wa kukabiliana na mashambulizi yoyote yanayoweza kutekelezwa na Russia.
Shirika la habari la Reuters limeandika: Ulaya ina wasiwasi na kupungua himaya ya kijeshi ya Marekani, na ndio maana inazidisha bajeti yake ya ulinzi.
Reuters imeashiria uwepo wa wanajeshi wa Marekani barani Ulaya tangu wakati wa Vita vya Pili vya Dunia na kuongeza kuwa: Marekani imeelekeza macho yake yote katika eneo la Asia-Pacific na suala hili ndilo linaloitia wasiwasi Ulaya.
Shirika la habari la IRNA pia limeripoti kuwa, katika hali ambayo aghalabu ya nchi za Ulaya zina matatizo ya nakisi ya bajeti, Umoja wa Ulaya unataka kuzidishwa bajeti ya ulinzi ya nchi hizo kwa asilimia 3.5 ya pato la taifa.
Kitambo nyuma, Umoja wa Ulaya ulitaka kuzidishwa bajeti ya ulinzi ya wanachama wake kwa asilimia 3.5 ya pato la taifa, hata hivyo hili halikufanikiwa kutokana na nchi nyingi za umoja huo kushindwa kutimiza lengo hilo.
342/
Your Comment