27 Machi 2025 - 15:47
Source: Parstoday
Siku ya Quds, Jihadul Islami yasisitiza: Muqawama bado una nguvu

Ziad Al-Nakhala, Katibu Mkuu wa harakati ya Jihadul Islami ya Palestina ametoa hotuba kwa mnasaba wa maandalizi ya Siku ya Kimataifa ya Quds akiwapongeza mashahidi wa Operesheni Kimbunga cha al Aqsa na kusema: "Malengo yetu ni ya hali ya juu na adhama yetu ni kubwa. Wazayuni wauaji na washirika wao hawawezi kuvunja irada yetu, na tunazidi kuwa na nguvu. Muqawama wetu unaweka historia isiyosahaulika leo hii."

Katibu Mkuu wa harakati ya Jihadul Islami ya Palestina aidha amesema: "Umoja na mshikamano wa vikosi vya Muqawama katika eneo hili bado upo." Taifa letu limethibitisha kuwa licha ya njama zote za kimataifa, lakini bado lina nguvu na haliwezi kushindwa. Quds ni kubwa kuliko silaha zote duniani."

Hayo yamekuja hukuru Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palesitna HAMAS ikiwa imeonya kwamba mashambulizi ya kiholela yanazofanywa na utawala ghasibu wa Israel yanahatarisha maisha ya mateka wa Kizayuni na ni uendelezaji wa hatua zilizoshindwa za Benjamin Netanyahu za kutaka kuwaachilia huru kwa nguvu mateka hao.

Hayo yamo kwenye taarifa ya jana Jumatano ya HAMAS ambayo imesema: "Kurejea vitani ni uamuzi uliokuwa umeshachukuliwa tangu zamani na Benjamin Netanyahu, ili kuvuruga makubaliano hayo na kusalimu amri mbele ya usaliti wa Itamar Ben Gvir"

Siku ya Quds, Jihadul Islami yasisitiza: Muqawama bado una nguvu

Hamas imeongeza kuwa: "Netanyahu anabeba dhima yote ya kuvurugika makubaliano hayo, na jamii ya kimataifa na wapatanishi wanapaswa kumshinikiza akomeshe jinai na mauaji yake na arejee kwenye mchakato wa mazungumzo."

Taarifa ya Hamas imesema: "Muqawama unafanya kila uwezalo kulinda maisha ya mateka wa Israel, lakini mashambulizi ya kiholela ya adui Mzayuni yanahatarisha maisha yao."

Hamas imeongeza kwa kusema: "Netanyahu anazidanganya familia za mateka wa Kizayuni anapoziambia kwamba mashambulizi ya kijeshi yanaweza kuwarejesha wakiwa hai. Kila wakati wavamizi hao walipojaribu kuwarudisha mateka wao kwa nguvu za kijeshi, wamekuwa wakipokea tu miili ya mateka hao kwenye majeneza.

Huku ukiwa unaungwa mkono kikamilifu na Marekani, utawala katili wa Israel, ulianzisha vita vikali dhidi ya wakaazi wa Ukanda wa Ghaza tarehe 7 Oktoba 2023 hadi Januari 19, 2025 ukiwa umesababisha uharibifu mkubwa na hasara nyingi za roho za watu wasio na hatia. Lakini pamoja na hayo jinai zote hizo hazikuwawezesha Wazayuni kufikia malengo yao waliyoyatangaza. Siku chache zilizopita, utawala huo umeanzisha wimbi jipya la mashambulizi huko Ghaza na hadi sasa umeshaua shahidi na kujeruhi idadi kubwa ya Wapalestina wasio na hatia.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha