27 Machi 2025 - 15:48
Source: Parstoday
Balozi wa Iran akosoa kuenea chuki dhidi ya Uislamu katika nchi za Magharibi

Ali Bahraini, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Geneva, amekosoa kuenea kwa chuki dhidi ya Uislamu au kwa maneno mengine Islamophobia katika nchi za Magharibi

Bahraini, ambaye alikuwa akizungumza katika kikao kilichofanyika katika Makao Mkauu ya Umoja wa Mataifa kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Kupmabana na chuki dhidi Uislamu amesisitiza kwamba "Chuki dhidi ya Uislamu" ni hofu isiyoelezeka na isiyo ya mantiki kuhusu uwepo na kuenea kwa Uislamu katika jamii ambazo kwa kiasi kikubwa si za Kiislamu.

AkizungumzaJ umanne katika kikao hicho, kilichoitishwa na nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC), amesema serikali zina jukumu la kukabiliana na tatizo hilo.

Umoja wa Mataifa mnamo 2022 ulitoa azimio, ukitaja tarehe 15 Machi kuwa Siku ya Kimataifa ya Kupambana na chiki dhidi ya Uislamu. Iran ilikuwa miongoni mwa waanzilishi wa azimio hilo na ilifanya juhudi nyingi katika kuandaa rasimu na kuhakikisha limepitishwa. Tangu wakati huo, kila mwaka mnamo tarehe 15 Machi, mada ya chuki dhidi Uislamu na matokeo ya kukabiliana nao hupigiwa kura na kujadiliwa na viongozi wa nchi mbalimbali.

Kwa kweli, kuenea kwa sera za chuki dhidi ya Uislamu katika nchi za Magharibi kumekuwa moja ya wasiwasi mkubwa kwa nchi mbalimbali, hasa zile za Kiislamu na pia Waislamu wanaoishi katika nchi hizo za Magharibi.

Nchi za Magharibi kwa miaka mingi zimekuwa zikitekeleza sera za chuki dhidi Uislamu kama moja ya sera zao za kuwashinikiza Waislamu. Katika miaka ya hivi karibuni, sera hizo zimepanuka, ambapo viongozi wa nchi za Magharibi wanatumia majukwaa mbalimbali kufikia hilo, wakieneza chuki dhidi ya Uislamu na kujaribu kuhamasisha mawazo ya umma dhidi ya Waislamu

Balozi wa Iran akosoa kuenea chuki dhidi ya Uislamu katika nchi za Magharibi

Viongozi wa nchi za Magharibi mara nyingi wanawatuhumu Waislamu kuwa chanzo cha matatizo kama vile ugaidi, ukosefu wa ajira na ghasia ambapo wengi wao katika hotuba zao huchochea vurugu dhidi ya Waislamu. Katika nchi za Ulaya, hasa Ufaransa, ambazo zinadai kuheshimu haki na uhuru wa kibinadamu, wanawake Waislamu mara nyingi hukabiliwa na mashinikizo na hata kukutana na vizuizi na marufuku za kisheria kutokana na uamuzi wao wa kuvaa mavazi yao ya staha ya Kiislamu.

Huko Marekani, Rais Donald Trump wa nchi hiyo, ni kinara rasmi wa chuki dhidi Uislamu nchini Marekani na ulimwengu wa Magharibi kwa ujumla. Trump mara kwa mara amekuwa akitoa matamshi dhidi ya Waislamu na tayari ametangaza kuendeleza ile sera yake ya awamu ya kwanza ya  kupiga marufuku raia wa nchi kadhaa za Kiislamu kuingia Marekani.

Mashambulizi dhidi ya misikiti na kuchoma maeneo ya ibada ya Kiislamu, mashambulizi ya kimwili na ya matamshi dhidi ya Waislamu, ubaguzi dhidi ya wafuasi wa Uislamu katika masuala mbalimbali ya elimu na kazi, na kukabiliana na wahamiaji Waislamu ni baadhi tu ya mifano ya chuki dhidi ya Uislamu katika jamii za Magharibi na hayo yote yamesababisha ongezeko la vurugu zisizo za kawaida dhidi ya Waislamu.

Balozi wa Iran akosoa kuenea chuki dhidi ya Uislamu katika nchi za Magharibi

Ripoti mpya zinaonyesha kwamba dhana ya chuki dhidi ya Uislamu katika nchi za Ulaya na Amerika Kaskazni imeongezeka sambamba na vita vya Gaza na mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina yanayotekelezwa na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Katika muktadha huu, Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, katika ujumbe wake katika Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Chuki dhidi ya Uislamu mwaka huu,  bila kutaja nchi au serikali yoyote, alisema “Tunashuhudia ongezeko la kutia wasiwasi la chuki dhidi ya Uislamu. Kuanzia kueneza wasifu wa kimbari na sera za kibaguzi zinazokiuka haki na utu wa mwanadamu, hadi unyanyasaji wa moja kwa moja dhidi ya watu binafsi na maeneo ya ibada. Hii ni sehemu ya janga kubwa la kutovumiliana, itikadi kali na mashambulizi dhidi ya makundi ya kidini na watu walio hatarini.”

Inaonekana kwamba chuki dhidi ya Uislamu katika nchi za Ulaya na Amerika Kaskazini sasa ni silaha ya kisiasa ambayo mbali na kuathiri maisha ya Waislamu, imeongeza mvutano wa kijamii na kisiasa katika nchi mbalimbali na hata katika kiwango cha kimataifa.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha