31 Machi 2025 - 22:06
Source: Parstoday
Rais wa Iran: Mwelekeo wa mazungumzo unategemea mwenendo wa Wamarekani

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa Tehran haijawahi kukwepa mazungumzo, lakini ni aina ya mwenendo wa Wamarekani ndio unaoamua ikiwa mazungumzo yataendelea au la.

Kwa mujibu Shirika la Habari la la IRIB, Masoud Pezeshkian, Rais wa Iran, siku ya Jumapili katika kikao cha baraza la mawaziri alizungumzia barua ya Donald Trump, Rais wa Marekani kwa Iran, na kusema: “Mazungumzo ya moja kwa moja kati ya pande mbili hayajaafikiwa, lakini njia ya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja bado iko wazi. Imesisitizwa kuwa Iran haijawahi kukataa mazungumzo, na ukiukwaji wa mapatano lazima ufidiwe na uaminifu uweze kurejeshwa.”

Rais wa Iran amewashukuru wananchi wa Iran kwa ushiriki wao wenye hamasa na dhamira thabiti katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds. 

Aidha Rais Pezeshkian amewapongeza wananchi wote wa Iran na Waislamu wa duniani kwa mnasaba wa Sikukuu ya Idul Fitr. Ameelezea matumaini yake kuwa mwezi mmoja wa kujisafisha nafsi na ibada umechangia kuboresha mwenendo, mazungumzo na tabia za kijamii na za mtu binafsi.

Rais wa Iran pia amesema kuwa uhalifu mbaya unaotekelezwa na utawala wa Kizayuni lazima ukomeshwe, akisisitiza kuwa: “Hali hii haikubaliki kamwe ambapo licha ya kutangazwa kwa usitishaji vita, bado wanawadondoshea mabomu watu wasio na hatia kwa kutumia zana na teknolojia za kisasa. Hakuna binadamu mwenye heshima anayekubali tabia hii isiyo ya kibinadamu.”

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha