Huku kukiwa na mporomoko wa haki za binadamu, ukata mkubwa wa kifedha na ubaguzi uliokithiri, wengi wameamua kuhamia katika mji mkuu wa Mexico, ambao umekuwa ukikaribisha idadi kubwa ya Wamarekani tangu wakati wa mlipuko wa janga la COVID-19.
Wamarekani milioni moja wanaishi Mexico, ambao ni sawa na takriban 20% ya Wamarekani milioni 5 waliohamia nje ya nchi hiyo, kwa mujiibu na sensa ya 2023 iliyochapishwa na shirika linalotetea maslahi yao.
Tiffany Nicole, 45, alihamia Mexico City baada ya polisi wa Marekani kumuua Mmarekani mwenye asili ya Afrika, George Floyd, Mei 2020.
"Sijisikii salama tena katika nchi yangu kama mtu mweusi," amesema mshauri huyo wa masuala ya kifedha na kuongeza kwamba, alikuwa akifikiria kurejea Chicago ili kuwa karibu na binti yake, lakini ushindi wa Trump umekatiza matumaini yake.
Tangu Donald Trump arejee katika Ikulu ya White House mwezi Januari, Trump alitoa amri ya kuondolewa kaulimbiu ya kupigania haki za watu weusi ya Black Lives Matter, ambayo ilishika kasi baada ya mauaji ya George Floyd.
Jimenez, mwenye umri wa miaka 38 kutoka New York ambaye anafanya kazi kama mwalimu wa yoga na mshawishi wa michezo aliyeondoka Marekani mwaka wa 2022, anasema: Katika kipindi hiki cha uongozi wa Donald Trump, ukatili na ukandamizaji umeongezeka zaidi dhidi ya Wamarekani weusi, Walatino, Wadominika na kadhalika."
342/
Your Comment