31 Machi 2025 - 22:11
Source: Parstoday
Waziri Mkuu wa Greenland amjibu Trump: Marekani haitakipata kisiwa hiki

Waziri Mkuu wa Greenland amejibu matamshi ya Rais wa Marekani aliyedai kwamba Washington inataka kukidhibiti kisiwa hicho kikubwa cha ncha ya kaskazini ya dunia, na kusisitiza kwamba: "Marekani haitaipata Greenland".

Jens Frederik Nielsen ameeleza hayo katika ujumbe alioweka kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa X na kusema: "Donald Trump anasema Marekani imo mbioni kuitwaa Greenland, lakini nieleze kinagaubaga kwamba Marekani haitakipata kisiwa hiki."

Nielsen ameendelea kutilia mkazo uhuru na kujitawala kwa Greenland, na kuongezea kwa kusema: "sisi hatuna mfungamano na mtu mwingine yeyote na ni sisi wenyewe ndio tunaoamua mustakabali wetu".

Katika mahojiano na NBC News yaliyopeperushwa Jumapili asubuhi, Trump alizungumzia alichoeleza kuwa ni uhakika alionao wa 100% kwamba Greenland itaunganishwa na Marekani na wala hakuondoa uwezekano wa kuchukua hatua za kijeshi kufanikisha suala hilo.

Trump alisema, "kuna uwezekano mkubwa wa kuwa na Greenland bila kutumia nguvu za kijeshi," na akaongeza kwamba, "lakini siondoi uwezekano wa kuchukua hatua yoyote kwa ajili ya kukimiliki kisiwa hicho, na siondoi chaguo lolote lile mezani."

Rais wa Marekani ametoa matamshi hayo wakati makamu wake JD Vance alifanya safari iliyoibua makelele katika kisiwa cha Greenland siku ya Ijumaa.

Greenland ni eneo la kimkakati kijiografia na lina rasilimali nyingi za madini. Kisiwa hicho ndicho njia fupi zaidi ya kuunganisha Ulaya na Amerika ya Kaskazini na lina umuhimu kwa mtambo wa Marekani wa utoaji indhari ya mashambulizi ya makombora la balestiki.../

/342

Your Comment

You are replying to: .
captcha