3 Aprili 2025 - 18:05
Source: Parstoday
Onyo Kali la Iran kwa Marekani na Utawala wa Kizayuni

Katika mazingira ya kuongezeka kwa vita vya kisaikolojia vinavyoendeshwa na Marekani pamoja na utawala wa Kizayuni, na vitisho vya mara kwa mara kutoka kwa Donald Trump na maafisa waandamizi wa usalama wa utawala wake huko Washington kuhusu uwezekano wa kushambulia Iran iwapo kutakosekana makubaliano kuhusu suala la nyuklia, Tehran imetoa onyo kali kwa Marekani na Israel kuhusu madhara makubwa ya hatua yoyote ya kijeshi dhidi ya Iran.

Ali Larijani, mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na mwanachama wa Baraza la Kuainisha Maslahi ya Mfumo, alisema usiku wa Jumatatu tarehe 31 Machi kuwa iwapo Marekani au Israel wataishambulia Iran kijeshi kwa kisingizio cha nyuklia, basi Iran italazimika kuelekea kwenye utengenezaji wa bomu la nyuklia. Alisema wananchi watashinikiza kuanzishwa kwa mpango huo wa kuunda bomu la nyuklia. Aliongeza kuwa hatua yoyote ya kijeshi dhidi ya Iran haitakuwa na matokeo mepesi. Aidha amekosoa  barua ya Trump kwa Iran akisema haijatoa kitu kipya zaidi ya maneno yake ya kawaida yasiyo na msingi.

Larijani amesisitiza kuwa kauli za Trump hazichukuliwi kwa uzito mkubwa na wanasiasa wengi duniani, kwani wanazioni kama propaganda tu. Aidha amesema kuwa jeshi la Iran liko tayari kwa lolote linaloweza kutokea.

Mnamo Februari 4, 2025, Trump alidai yuko tayari kuzungumza na Rais wa Iran huku akisaini waraka wa kuendeleza sera ya “mashinikizo ya juu” dhidi ya Iran. Baada ya hapo alituma barua kwa Kiongozi Muadhamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, akitoa muhula wa  miezi miwili kufikia makubaliano mapya ya nyuklia la sivyo atachukua hatua za kijeshi dhidi ya Iran. Siku moja tu baada ya barua hiyo kuwasili Tehran, Wizara ya Hazina ya Marekani iliweka jina la Waziri wa Mafuta wa Iran, Mohsen Paknejad, kwenye orodha ya vikwazo.

Onyo Kali la Iran kwa Marekani na Utawala wa Kizayuni

Trump

Trump, akifuata sera ya “amani kupitia mabavu,” alitoa masharti mengi kwa Iran yakiwemo kusitisha misaada kwa harakati za Muqawama zinazoupinga utawala wa Kizayuni, kuacha mpango wa makombora na kusitisha ustawi wa teknolojia ya droni za kivita, pamoja wa silaha zisizo za kawaida na hata za kawaida , huku akiendeleza vitisho na mashinikizo.

Iran tayari imepata uzoefu mbaya na Marekani, hasa wakati wa kipindi cha kwanza cha Trump  wakati alipojiondoa kwenye makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kuanzisha vikwazo vikali dhidi ya Iran. Katika mahojiano yake, Larijani alisema kuwa Kiongozi Muadhamu hakukubali JCPOA kuwa ni makubaliano mazuri kwa kuwa Marekani iliweza kuyavunja kwa urahisi bila kujali kuwa Iran imetekeleza majukumu yake.

Vitisho vya kijeshi vya Trump, pamoja na kupelekwa kwa meli za kivita kama " USS Harry Truman" kwenye Bahari Nyekundu na "Carl Vinson" kwenye eneo la Ghuba ya Uajemi, pamoja na kuweka ndege za kivita za kisasa aina ya B2 katika kisiwa cha Diego Garcia, havitatisha Iran bali vinaimarisha dhamira ya viongozi wa Tehran kujibu kwa nguvu.

Ayatullah Khamenei amesema wazi kwamba msimamo wa Iran haujabadilika na iwapo uhasama wowote utatekelezwa, jibu kali litatolewa. Iran imeonya kuwa huenda sera yake kuhusu silaha za nyuklia ikabadilika iwapo itashambuliwa. 

Onyo Kali la Iran kwa Marekani na Utawala wa Kizayuni

Kombora la Emad la Iran

Ali Larijani, katika mahojiano yake na televisheni ya Iran, alisistiza: “Kufanya mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Iran hakutakuwa na athari ndogo. Fatwa ya Kiongozi wa Mapinduzi inasisitiza marufuku ya kuwa na silaha za nyuklia. Lakini, iwapo Marekani au Israel zitatumia kisingizio cha nyuklia kuishambulia Iran, basi Iran italazimika kuelekea kwenye utengenezaji wa bomu la nyuklia.”

Nukta nyingine ambayo Larijani alisisitiza ni kuwa: “Mpango wa nyuklia wa Iran hauwezi kuharibiwa kwa mabomu. Teknolojia ya nyuklia ya Iran imeundwa kwa njia ambayo hata baada ya mashambulizi ya mabomu, haitaathiriwa wala kucheleweshwa.”

Your Comment

You are replying to: .
captcha