Aleksey Andreev, Mwakilishi wa Biashara wa Russia nchini Morocco amesema hayo na kuongeza kuwa, katika hali ambayo Afrika ina utajiri mkubwa wa rasilimali, lakini data imekuwa rasilimali yenye thamani kubwa zaidi katika dunia ya sasa.
Ameeleza kuwa, Russia haina azma ya kunyonya rasilimali hizo, lakini inapania kuyapa mataifa ya Afrika zana za kuzisimamia na kuzilinda.
''Russia inatoa sio tu bidhaa za programu, lakini pia mfumo wa ikolojia wa suluhu za kidijitali ambazo zinahakikisha uhuru na ukuaji wa kiteknolojia," ameongeza.
Aidha Mwakilishi wa Biashara wa Russia nchini Morocco amebainisha kuwa, "Russia iko tayari kuwa mshirika wa kimkakati wa Morocco katika utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa kidijitali chini ya kampeni ya Morocco Digital 2030."
Amekumbusha kuwa, kuwa nchi wanachama wa kundi la BRICS zinachunguza hatua kadhaa za ubunifu wa kifedha ikiwemo kuanzisha mfumo wa malipo wa kidijitali ili kutoa huduma za kifedha ndani ya kambi hiyo ya kiuchumi.
Aleksey ameongeza kuwa, tofauti na kampuni nyingi za Magharibi, wawekezaji wa Russia wanafadhilisha ujanibishaji kuliko kubuni mifumo migumu ya utoaji wa leseni.
342/
Your Comment