Rais Pezeshkian amesema hayo katika mazungumzo ya simu na Rais Kais Saied wa Tunisia Jumatano usiku na kusisitiza kuwa, umoja wa nchi za Kiislamu unaweza kuzipa uwezo wa kuwaunga mkono watu wanaodhulumiwa wa Palestina ipasavyo.
Sanjari na kutoa pongezi kwa Rais na watu wa Tunisia kwa mnasaba wa Idul-Fitri, Dakta Pezeshkian ameshukuru na kupongeza uungaji mkono usioyumba wa Tunisia kwa kadhia ya Palestina.
Pezeshkian ameeleza kuthaminiwa na Iran misimamo ya kibinadamu ya Tunisia na kueleza matumaini yake kuwa, mataifa ya Kiislamu yanaweza kuungana katika juhudi zao za kukomesha ukatili unaofanywa na utawala dhalimu wa Kizayuni dhidi ya wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina.
Kwingineko katika matamshi yake, ameashiria dhamira ya Iran katika kuimarisha uhusiano na mataifa ya Kiislamu ikiwemo Tunisia.
Rais wa Tunisia kwa upande wake amempongeza mwenzake wa Iran na wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu kwa mnasaba wa sikukuu ya Idul-Fitr.
Kais Saied amesisitiza uungaji mkono madhubuti wa watu wa Tunisia kwa watu wasio na hatia wa Palestina na kuelezea matumaini yake kuwa hivi karibuni wataanzisha nchi huru, mji mkuu wake ukiwa ni Al-Quds.
342/
Your Comment