Katika taarifa yake leo Alkhamisi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baghaei amesema jinai za utawala wa Israel ni pamoja na mauaji yaliyopangwa ya waandishi wa habari, mashambulizi ya kimakusudi dhidi ya wafanyakazi wa afya na vituo vya afya, na uvamizi unaofanywa na walowezi wenye itikadi kali katika eneo la Msikiti wa al-Aqsa.
Ameongeza kuwa, nchi zote zinalazimika kuchukua hatua ili kukomesha siasa za Israel za kutumia njaa kama mojawapo ya njia za kufanikisha mauaji ya halaiki.
Msemaji huyo wa Iran amekosoa utepetevu wa baadhi ya nchi za Magharibi, zikiwemo Uingereza, Canada, Ujerumani na Ufaransa, juu ya ukiukaji wa "dhahiri na wa kimfumo" wa Israel wa haki za binadamu huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
"Kimya cha nchi hizi za Magharibi dhidi ya jinai za utawala ghasibu wa Israel ni ishara tosha ya unafiki wao kuhusiana na haki za binadamu na utawala wa sheria," amesisitiza.
Wanahabari ni miongoni mwa Wapalestina waliouawa shahidi Gaza
Baghaei amebainisha kuwa, nchi zote zina jukumu la pamoja la kuzuia na kukabiliana na jinai za kutisha za Israel, yakiwemo mauaji ya halaiki na uhalifu wa kivita, kwa kuzingatia sheria za kimataifa. Amesema kutoadhibiwa utawala wa Tel Aviv kumeupa kiburi na motisha zaidi wa kuendelea na mauaji ya watu wa Palestina na kukalia kwa mabavu ardhi za Wapalestina.
Aidha Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ametoa wito kwa mataifa yote hususan nchi za Kiislamu kushikamana na wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina ili kukomesha mauaji zaidi ya wanawake na watoto wasio na hatia.
342/
Your Comment