Katika wiki za hivi karibuni, vitisho vya vyombo vya habari vya Kiebrania na vita vya kisaikolojia dhidi ya Iran vimepamba moto tena, huku Wazayuni wakijaribu kuandaa mazingira ya kutaka ionekane kuwa Iran sasa imedhoofika sana na inaweza kudhurika kirahisi.
Vyombo hivyo vya habari vimekuwa vikizikuza jumbe na kauli za vitisho za Rais wa Marekani na harakati za jeshi la nchi hiyo katika eneo hili, na kutaka ihisike kuwa mashambulizi ya kijeshi ya Marekani dhidi ya Iran yanakaribia kufanywa na yanaweza kutokea wakati wowote ule kutoka sasa.
Hata hivyo katika sehemu ya mahojiano na televisheni ya hapa nchini, Dkt. Ali Larijani, Spika wa zamani wa Bunge na Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alijibu vitisho hivyo na kuwaonya Wamagharibi kwamba endapo watajaribu kuchukua hatua kama hiyo, wajue kwamba mwongozo inaofuata Iran katika masuala ya nyuklia utabadilika na hata wananchi pia watadai ziundwe silaha za nyuklia.
Baada ya kutangazwa msimamo huo ambao ulikuwa ishara ya wazi kwa jumbe za vitisho za Wazayuni na Marekani, kauli ya Dakta Ali Larijani imetoa mtikisiko mkubwa kwa kuakisiwa kwa wingi katika kurasa za magazeti na vyombo vya habari vya lugha ya Kiebrania.../
342/
Your Comment