3 Aprili 2025 - 18:09
Source: Parstoday
Araqchi: Iran haina lengo la kumiliki silaha za nyuklia

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu haitaki kuunda na kumiliki silaha za nyuklia kwa hali yoyote ile.

Sayyid Abbas Araqchi ameandika katika ukurasa wake wa X kwamba: Rais wa Marekani huwenda asipendezwe na makubaliano ya nyuklia ya 2015; lakini makubaliano hayo yanajumuisha jukumu muhimu la Iran ambalo bado lipo; na hata Washington ambayo imejitoa katika makubaliano hayo, imefaidika nalo.

Hakuna hata ushahidi mdogo kwamba Iran imekiuka ahadi na majukumu yake, hata baada ya miaka kumi tangu kusainiwa makubaliano ya JCPOA, na miaka 7 baada ya Marekani kujitoa kwa upande mmoja katika makubaliano hayo. 

Hivi majuzi Tulsi Gabbard, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa wa Marekani  alikiri pia kuhusu suala hili. 

"Mazungumzo ya kidiplomasia yamethibitisha kuwa na taathira, na bado yanaweza kuwa na taathira. Lakini inapaswa kubainika wazi kwa kila mtu kwamba, kimsingi hakuna kitu kama "chaguo la kijeshi", achilia mbali "suluhisho la kijeshi", amesema Sayyid Abbas Araqchi. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameongeza kuwa: Kushindwa pakubwa katika eneo la Asia Magharibi kwa serikali zilizotangulia za Marekani zilizotumia gharama ya zaidi ya dola trilioni 7 katika vita, mauaji na uvamizi wake wa kijeshi, ni kielelezo tosha. 

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha