3 Aprili 2025 - 18:11
Source: Parstoday
Guterres asisitiza kutekelezwa usitishaji vita haraka huko Gaza/ Iran pia yatoa wito wa kuchukuliwa hatua kimataifa kusitisha mauaji ya kimbari dhidi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametaka kurejea haraka iwezekanavyo katika makubaliano ya kusitisha vita katika Ukanda wa Gaza.

Antonio Guterres kwa mara nyingine tena ametaka kurejea haraka iwezekanavyo katika makubaliano ya kusimamisha mapigano katika Ukanda wa Gaza na kutaka kuachiwa huru bila ya msharti mateka na kusambazwa bila vizuizi misaada ya kibinadamu katika Ukanda wote wa Gaza.  

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema: Mashambulizi makubwa ya anga ya Israel na operesheni za ardhini za utawala huo katika muda wa siku mbili zilizopita pekee zimesababisha uharibifu mkubwa na kufurushwa kwa Wapalestina zaidi ya 100,000 katika mji wa  Rafah. 

Katibu Mkuu wa UN amekosoa shambulio la  jeshi la Israel dhidi ya msafara wa wafanyakazi wa sekta ya tiba na huduma za dharura la Machi 23 mwaka huu lililouwa wafanyakazi wa tiba na wa huduma za misaada 15 katika Ukanda wa Gaza na kuongeza kuwa: Tangu Oktoba 2023, wafanyakazi wasiopungua 408 wameuawa huko Gaza, 280 kati yao wakiwa ni wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa.

Wakati huo huo Esmail Baqaei Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran leo Alhamisi ameashiria ripoti ya karibuni ya Ripota wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa anyehusika na masuala ya haki ya chakula ambaye ametaka Israel ishinikizwe ili isimamishe sera zake za kutumia njaa kama wenzo  mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina na kubainisha masikitiko yake kufuatia kunyamaza kimya nakutochukua hatua zozote baadhi ya nchi za Magharibi zinazodai kutetea haki za binadamu duniani zikiwemo Uingereza, Canada, Ujerumani na Ufaransa mkabala wa ukiukwaji mkubwa na wa kimfumo wa haki za binadamu unaofanywa na Israel katika Ukanda wa Gaza.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha