Volker Turk amesema hayo baada ya Israel kufanya ukatili mwingine wa kuua madaktari 15 na wafanyakazi wa dharura huko Ghaza na kuzua wasiwasi mkubwa kuhusu uhalifu wa kivita unaofanywa na jeshi la utawala wa Kizayuni.
Volker Turk ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba: "Nimeshtushwa na mauaji ya hivi karibuni ya wafanyikazi 15 wa matibabu na wasaidizi wao, ambayo yanazua wasiwasi zaidi kuhusu uhalifu wa kivita unaofanywa na jeshi la Israel,"
Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu ameongeza kwamba: "Lazima kufanyike uchunguzi huru, wa haraka na wa kina kuhusu mauaji haya. Wale wanaohusika na ukiukaji wowote wa sheria za kimataifa lazima wawajibishwe."
Matamshi hayo yamekuja huru vyombo vya habari vya Palestina vimeripoti kuwa katika jinai ya karibuni zaidi, Israel imeshambulia zahanati ya Umoja wa Mataifa katika kambi ya Jabalia kaskazini mwa Ukanda wa Ghaza ambako wakimbizi wa Kipalestina wanahifadhiwa.
Takriban watu 22, wakiwemo watoto na askari wa jeshi la polisi la Ghaza, wameuawa shahidi katika shambulio hilo lililopiga zahanati ya Umoja wa Mataifa.
Utawala wa Kizayuni, kwa uungaji kamili wa Marekani ulianzisha vita vya kutisha dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Ghaza tarehe 7 Oktoba, 2023 hadi Januari 19, 2025 na kusababisha uharibifu mkubwa wa roho na mali lakini ilishindwa kufikia malengo yake kutokana na Muqawama wa kihistoria wa wananchi wa Ghaza.
342/
Your Comment