4 Aprili 2025 - 23:18
Source: Parstoday
Vikosi vya Yemen vyatungua ndege isiyo na rubani ya Marekani MQ-9

Jeshi la Yemen limeitungua ndege isiyo na rubani ya MQ-9 ya Marekani wakati ilipokuwa inafanya mashambulizi ya kiuadui katika anga ya mkoa wa Hodeidah. Hiyo ni droni ya 17 kutunguliwa na Jeshi la Yemen kama sehemu ya vita vitakatifu vya Jihad vya kuwaunga mkono wananchi wa Ghaza.

Taarifa iliyotolewa Alkhamisi na Jeshi la Yemen dakika chache baada ya kutunguliwa ndege hiyo ya Marekani imeeleza kuwa: Wanajeshi wa Yemen wameiangusha ndege isiyo na rubani ya MQ-9 ya Marekani iliyokuwa inafanya mashambulizi ya kiuadui katika anga ya mkoa wa Hodeidah nchini Yemen. Droni hiyo ya Marekani imeangushwa kwa kutumia kombora la ardhini kwa angani.

Brigedia Jenerali Yahya Saree, Msemaji wa Jeshi la Yemen amebainisha katika taarifa hiyo kwamba: "Kikosi cha Ulinzi wa Anga cha Wanajeshi wa Yemen, kimejibu mashambulizi ya Marekani nchini Yemen kwa kutungua droni ya MQ-9 ya Marekani ikiwa ni muendelezo wa Vita vya Jihadi vya wananchi wa Yemen vya kuwaunga mkono ndugu zao Wapalestina."

Msemaji wa Jeshi la Yemen aidha amesema: "Droni hiyo ya Marekani imepigwa kwa kombora lililotengenezwa na wananchi wenyewe Yemen la kushambulia vifaa vya angani kutokea ardhini."

Amesema: "Hii ni ndege ya pili isiyo na rubani ambayo Jeshi la Anga la Yemen limefanikiwa kuitungua ndani ya saa 72, na ni droni ya 17 kutunguliwaa na Jeshi la Yemen."

Taarifa hiyo imesema: "Vikosi vya Yemen vinasisitizia kuendelea kupinga njama zote za adui za kujaribu kudhoofisha mamlaka ya nchi yao na vitaendeleza operesheni za kuwaunga mkono wananchi wa Ghaza."

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha