Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Samahat Sheikh Dr.Abdur_ Razak Amiri ameeleza na kufafanua juu ya suala la Malezi kwa Watoto katika Jamii kuwa ni suala la Baba na Mama.
Lakini kwa sasa tumezoea kusikia Lugha ya Single Mother. Ipo nchi moja Duniani ina Wanawake ambao ni Single Mother Milioni 6.
Na asilimia 80% ya Watoto wanaozaliwa na kulelewa katika familia za namna Ile (Familia za Ma_single Mother), hukosa maadili na malezi. Utaratibu wa Mwenyezi Mungu aliouweka, Mtoto hulelewa na Baba na Mama.
Nyumba ikikosa mmoja Baba au Mama, lazima kuwe na dosari katika Malezi ya Mtoto. Lakini kwa sasa hivi, usingle mother imekuwa ni fakhari kwa baadhi ya Wanawake, Mwanamke akiwa na uwezo unamkuta anajifakharisha kuwa Mimi ni Single Mother sitaki mambo ya kupelekwa pelekwa mbio, sitaki Mwanaume (Mume)!
Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa Mtoto 1 kati ya Watoto 5 amelelewa na Single Mother, maana yake kuna pungufu katika Malezi kwa Mtoto huyo.
Your Comment