Katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Sheria, ilibainika kuwa Rais Murmu alitia saini muswada huo ambao tayari ulikuwa umeidhinishwa na mabunge yote mawili—Lok Sabha na Rajya Sabha—wiki iliyopita.
Sheria hiyo imeibua upinzani mkali, huku uhalali wake ukipingwa mahakamani na kiongozi wa chama cha All India Majlis-e-Ittehadul Muslimeen (AIMIM), Asaduddin Owaisi, pamoja na Mbunge wa Congress, Mohammad Javed, waliowasilisha kesi katika Mahakama Kuu ya India.
Kwa upande mwingine, Mallikarjun Kharge, kiongozi wa upinzani katika Rajya Sabha, aliishutumu serikali ya chama tawala cha Bharatiya Janata Party (BJP) kwa kuchochea mgawanyiko wa kijamii kupitia muswada huo unaowalenga Waislamu.
Kabla ya kuidhinishwa kwa muswada huo, Kharge aliorodhesha kasoro nyingi na kuitaka serikali kuufuta. Alisema sheria hiyo ni "kinyume cha katiba" na inalenga kudhoofisha haki na usalama wa Waislamu waliowachache nchini India.
Wakati huo huo, Waislamu nchini humo wameingiwa na hofu kuwa magenge ya Kihindu yenye misimamo mikali yanaweza kutumia sheria hiyo kunyakua misikiti ya kihistoria kwa madai kwamba yalijengwa juu ya mahekalu ya Kihindu.
Mnamo Januari 2024, Waziri Mkuu Narendra Modi alizindua hekalu la Kihindu katika mji wa kaskazini wa Ayodhya, mahali palipokuwa msikiti wa kihistoria wa Babri uliojengwa katika karne ya 16.
Mnamo mwaka 1992, wanamgambo wa Kihindu waliubomoa msikiti huo wa zaidi ya miaka 400. Viongozi wa BJP walihusishwa moja kwa moja katika tukio hilo la kubomoa nyumba hiyo ya ibada. Baada ya uharibifu huo, machafuko ya kidini yaliibuka kati ya Wahindu na Waislamu, na kusababisha vifo vya watu wapatao 3,000.
342/
Your Comment