Katika ripoti yake mpya, shirika hilo linasema timu zake zimebaini maelfu ya uhalifu unaotekelezwa na jeshi la Israel, na kutoa ushahidi wa kutosha wa mauaji ya kimbari. Ripoti hiyo inasema, “Uhalifu huu unaonyesha kiwango cha juu cha ukatili ambacho hakijawahi kushuhudiwa katika historia ya hivi karibuni, kwa kiwango, malengo ya moja kwa moja, na nia ya kuangamiza watu.”
Shirika hilo linaongeza kuwa ukatili huu unazidi hata ule wa makundi ya kigaidi kama Daesh ISIS, huku lilitaja ukatili huo wa Israel dhidi ya Wapalestina kuwa ni "kampeni kubwa na ya kimfumo ya maangamizi ya kihistoria."
Ripoti hiyo pia inakosoa ukimya wa jumuiya ya kimataifa kuhusu mauaji haya, ikisema kuwa kimya hicho kinawafanya viongozi wa dunia kuwa washirika katika kile kinachoelezwa kama mauaji ya halaiki yaliyopangwa ya Wapalestina.
Katika tukio la karibuni, jeshi la Israel liliripua roboti iliyojaa vilipuzi katikati ya mtaa wenye watu wengi wa Shuja’iyya, Gaza Mashariki, ambapo hakuna mapigano wala sababu ya kijeshi kuwepo. Watu 21 waliuawa, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa.
Tangu mashambulizi ya Israel kuanza tena Gaza zaidi ya wiki tatu zilizopita, watoto 322 wa Kipalestina wameuawa na 609 kujeruhiwa. Kwa ujumla, watu 1,249 wameuawa tangu uvamizi mpya uanze, huku idadi ya majeruhi ikiwa ni 3,022.
Wizara ya Afya ya Gaza inasema kuwa tangu Israel ianzise vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza tarehe 7 Oktoba 2023, watu 50,609 wameuawa na 115,063 kujeruhiwa, wengi wakiwa ni wanawake na Watoto.
342/
Your Comment