Waandamanaji hao jana Jumatatu walikashifu sera za Netanyahu, ikiwa ni pamoja na hatua yake ya kuwatimua maafisa wakuu wa usalama na sheria wa utawala huo. Pia wamelaani kuanzishwa tena kwa vita vya mauaji ya halaiki dhidi ya watu wa Gaza.
Familia za mateka wa Israel wanaoshikiliwa huko Gaza pia walijiunga na maandamano hayo, wakihimiza kukomeshwa vita na kufikiwa makubaliano ya kuhakikisha kuachiliwa huru kwa mateka hao.
Maandamano hayo makubwa yalifuatia maandamano ya kila wiki siku ya Jumamosi ambapo waandamanaji wanalitaka baraza la mawaziri la utawala huo kutanguliza mbele suala la mateka juu ya maslahi mengine. Pia wameutaka utawala huo kuacha kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza na Harakati ya Hamas.
Harakati hiyo ya Muqawama ya Palestina ilisema itawaachilia huru mateka waliosalia ili kubadilishana na kuachiliwa kwa mateka zaidi wa Kipalestina, kufikiwa usitishaji vita wa kudumu, na Israel kujiondoa kabisa kutoka Gaza.
Israel ilihitimisha kwa upande mmoja makubaliano ya kusitisha mapigano ya Gaza na kuanza tena vita vyake vya mauaji ya halaiki dhidi ya watu wa Gaza mnamo Machi 18, ambapo hadi sasa idadi ya vifo imefikia 1,391, na wengine 3,434 wamejeruhiwa, kulingana na vyanzo vya matibabu.
342/
Your Comment