13 Aprili 2025 - 22:31
Source: Parstoday
Kiongozi Muadhamu: Adui amekatishwa tamaa na ana hofu na maendeleo ya Jamhuri ya Kiislamu

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Sayyid Ali Khamenei leo Jumapili mchana amekutana na baadhi ya makamanda wa jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa mnasaba wa Mwaka Mpya wa Kiirani wa Hijria Shamsia na kusisitiza kuwa, adui amekata tamaa vibaya na amekasirishwa na maendeleo ya Jamhuri ya Kiislamu. Wakati huo huo amesisitiza kwamba, pamoja na kuwepo mapungufu, lakini kuna maendeleo pia yamepatikana, inabidi hayo nayo tuyaone.

Akisisitizia kuendelea kuimarishwa utayari wa hali ya juu wa watu, vifaa na programu katika kutimiza jukumu hili la kitaifa kwa njia bora kabisa, Kiongozi Muadhamu amesema: "Maendeleo ya nchi yamewakasirisha na kuwakatisha tamaa maadui na wale wasioitakia kheri Iran. Tab'an, kuna mapungufu katika baadhi ya maeneo kama vile masuala ya kiuchumi ambayo bila ya shaka yanahitaji kushughulikiwa, lakini maendeleo pia yamepatikana, inabidi hayo nayo tuyaone.

Ayatullah Khamenei aidha amesema kwamba, utayari wa zana za vikosi vya ulinzi vya Iran ni lazima uendane na kuimarika uthabiti wa kiimani kuhusu malengo matukufu, majukumu na yakini juu ya haki ya njia tuliyochagua. Hili pia ni muhimu na ndio maana maadui wanafanya njama kubwa za kulitia doa suala hilo. 

Vilevile amesema kuwa, suala la Uislamu na uhuru ndani ya Jamhuri ya Kiislamu ndiyo mambo yanayowakasirisha mno maadui. Ameongeza kuwa: Kinachomuumiza sana adui si jina la Jamhuri ya Kiislamu bali ni nia na dhamira ya kweli ya nchi ya Kiislamu (kama Iran)  kupigania kuwa huru na kuwa na heshima na utambulisho wake wa kweli. 

Ayatullah Khamenei ametoa mfano wa siasa za kindumilakuwili za mabeberu wa dunia yaani suala la kumiliki silaha angamizi zaidi na haramu zaidi zinazofanya mauaji na kusababisha majanga makubwa ulimwengu na kusema: Yakini, imani, dhamira, ushujaa na kutawakali kwa Mwenyezi Mungu kunapaswa kuwe kwa hali ya juu mno ndani ya vikosi vya ulinzi kwani historia imeripoti kwamba, majeshi makubwa makubwa ambayo yalikuwa yamejizatiti kikamilifu kwa silaha nyinginezo lakini hayakuwa na silaha hii, yote yameshindwa. 

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha