Ismail Baghaei amesema hayo katika mahojiano maalumu na IRIB na kuongeza kwamba, mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani nchini Oman yataendelea.
Akijibu swali ambalo baadhi ya duru za habari zimeripoti kuwa rasimu ya Steve Whittaker, mwakilishi maalumu wa Marekani katika eneo la Asia Magharibi haikugusia suala jingine lolote kama la ushawishi wa Iran kwenye eneo hili na uwezo wake wa makombora, bali imejikita tu kwenye kadhia ya nyuklia, Baghaei amesema: "Tunapoangalia mawasiliano ya maandishi yaliyofanyika tangu mwanzo wa mchakato uliopelekea kufanyika mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati yetu na Marekani tutaona kuwa, msingi wa mawasiliano hayo haukuwa na chochote kingine ghairi ya suala la nyuklia. Kwa hivyo nadhani ni wazi kuwa upande wa Marekani umeingia kwenye mazungumzo hayo kwa mujibu wa maagizo yale yale iliyokuwa imepatiwa na Iran."
Akijibu uvumi wa kufanyika mazungumzo ya moja kwa moja, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: "Uvumi huu si wa kweli. Msingi wetu ulikuwa ni kile tulichojitolea kukifanya na ni kwa mujibu wa maagizo yaliyotolewa na ngazi za juu za Jamhuri ya Kiislamu. Maudhui pekee ilikuwa ni kuzungumza na Marekani kwa njia isiyo ya moja kwa moja tena kuhusu suala la nyuklia na kuondolewa kwa vikwazo tu."
342/
Your Comment