13 Aprili 2025 - 22:39
Source: Parstoday
Ripoti: EU inakabiliwa na mgogoro wa afya ya akili ya vijana

Mgogoro wa afya ya akili kwa vijana katika nchi za Umoja wa Ulaya (EU) unazidi kuongezeka. Mjadala katika Bunge la Ulaya umebaini kuwa asilimia 20, ambayo ni sawa na vijana milioni 14, sasa wanahangaika na matatizo ya kisaikolojia.

Serikali na taasisi za Umoja wa Ulaya zinashutumiwa kwa kupuuza tatizo hilo.

Inasemekana kuwa mkakati wa Tume ya Ulaya wa afya ya akili uliogharimu euro bilioni 1.2, ambao ulizinduliwa mnamo 2023, umeshindwa kuleta matokeo ya maana katika uwanja huu.

Vijana wa Ulaya wanasumbuliwa na mashinikizo makubwa wanapotatizika kupata kazi bora na nyumba za bei nafuu. Wakati huo huo, vijana wanakabiliwa na uonevu mtandaoni, matamshi ya chuki na maudhui yasiyofaa kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii.

Mwakilishi mmoja wa Bunge la Ulaya amesema: "Tuna visa vingi vya kujiua vijana na hakuna mfumo mzuri wa huduma ya afya ya bure."

Wakosoaji wanasema kuwa viongozi wa EU wanazingatia zaidi kufadhili vita kuliko kujali raia wao.

Wakosoaji wengine wanataja pombe, matumizi mabaya ya dawa za kulevya na kile wanachokiita ajenda ya uliberali wa hali ya juu, kama mambo yaliyochangia pakubwa katika mgogoro huo.

Kujiua sasa ni sababu ya pili ya vifo katika Uumoja wa Ulaya kati ya watoto wenye umri wa miaka 16 hadi 24, baada ya ajali za barabarani.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha