13 Aprili 2025 - 22:41
Source: Parstoday
CNN: Uvumilivu wa Wamarekani kwa Tel Aviv unaisha

Chanzo makini kimetangaza kuwa, subira ya Wamarekani kwa vitendo vya utawala wa Kizayuni wa Israel inakwisha.

Televisheni ya CNN ya Marekani imekinukuu chanzo kilichoshiriki katika mazungumzo ya kubadilishana mateka na mahabusi kati ya utawala wa Israel na harakati ya Hamas kikisisitiza kuwa, lengo la maafisa wa Israel katika kufanya mazungumzo hayo haliko wazi.

Chanzo hicho kimeongeza kuwa: "Uvumilivu wa Wamarekani katika suala hili unaisha na unakaribia kumalizika."

Chanzo hicho kimesema timu ya mazungumzo ya Tel Aviv inafanya mazungumzo na wawakilishi wa Hamas kwa malengo ya kisiasa.

Chanzo hicho kimeongeza kuwa Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amewaweka kando wataalamu wa masuala ya usalama katika mazungumzo hayo.

Awali duru za kuaminika zilisema kuwa Benjamin Netanyahu ambaye anaandamwa na kesi kadhaa za kisiasa na ubadhirifu wa mali ya umma mahakamani, anatumia vita vya Gaza mazungumzo na Hamas ili kuendelea kubakia madaraka.  

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha