Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Masuala ya Sheria na Kimataifa wa Iran, Kazem Gharibabadi, ametoa wito huo wakati wa kikao cha tatu cha uchunguzi wa mahakama ya ICJ kuhusu wajibu wa Israel kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayotoa misaada kwa Wapalestina huko Gaza.
Mwanzoni mwa matamshi yake, Gharibabadi ameangazia hadhi ya ICJ kama mamlaka ya juu zaidi ya kisheria ndani ya Umoja wa Mataifa, akibainisha kwamba chombo hicho cha kimataifa kwa mara nyingine kinakabiliwa na mtihani wa kihistoria, ambao unahusishwa moja kwa moja na hatima ya taifa linalodhulumiwa.
Akitoa ushahidi usiopingika wa mauaji ya kimbari yanayofanyika huko Gaza, mwanadiplomasia huyo wa Iran ameonya kwamba fursa ya kuzuia mauaji hayo makubwa ya kimbari inatoweka haraka.
"Licha ya amri kadhaa za Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu (ICJ), utawala wa Kizayuni wa Israel unaendelea na siasa zake mbaya, na jamii ya kimataifa imeshindwa kutekeleza wajibu wake wa kimaadili na kisheria", amesema Kazem Gharibabadi.
Akirejelea ripoti ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu na mashirika mengine ya kimataifa, Gharibabadi amesema kuwa upatikanaji wa misaada ya kibinadamu umezuiwa kikamilifu na haya ni mauaji ya kimbari ya moja kwa moja.
Vilevile ameashiria uchunguzi uliofanywa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) na Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu (ICJ) kuhusu hatua za viongozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel na kubainisha kwamba, kuna ushahidi wa kutosha wa kuthibitisha kutendeka jinai za kimataifa.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameiambia Mahakama ya Kimataifa ya Haki kwamba: "Kushindwa kufikishwa haraka misaada ya kibinadamu kwa watu wa Palestina ni ukiukaji wa wazi wa kanuni za kimataifa kuhusu kuzuia mauaji ya kimbari."
Majaji wa mahakama ya ICJ wanafanya vikao vya wiki moja ili kuandaa maoni ya ushauri juu ya wajibu wa Israel kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa huko Gaza.
342/
Your Comment