10 Mei 2025 - 22:07
Source: Parstoday
Israel yatumia njaa kama silaha ya vita huku Mabakeri yote Gaza yakifungwa

Utawala haramu wa Israel unaendelea kutumia njaa kama silaha ya vita huku taarifa zikisema unga wa ngano umemalizika kabisa katika Ukanda wa Gaza, na kusababisha kufungwa kwa mabakeri yote.

Abdel Nasser al-Ajrami, mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Mabakeri Gaza, ametoa kauli hiyo kwa Shirika la Habari la Palestina Safa, ambalo lilichapisha taarifa hizo Ijumaa.

Kwa mujibu wa afisa huyo, kufungwa huko kumetokana na uhaba mkubwa wa unga na mafuta, hali iliyoletwa na kuongezeka kwa mzingiro wa utawala wa Israel dhidi ya eneo hilo.

Utawala katili wa Israel ulianzisha vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza mnamo Oktoba 7 2023, kama jibu kwa operesheni ya kihistoria ya kulipiza kisasi wapigania ukombozi wa Palestina. Tokea wakati huo Isael imeua Wapalestina zaidi ya 52,700, wengi wao wakiwa wanawake na watoto. Wakati huohuo, utawala huo umeshadidisha  mzingiro wake ulioanza mwaka 2007 dhidi ya Gaza.

Shirika la misaada la World Central Kitchen lilitangaza Jumatano kuwa haliwezi tena kupika au kuandaa chakula kwa Wapalestina wa Gaza kutokana na kuisha kwa akiba ya chakula na mafuta yanayohitajika kwa kupika.

Wananchi wengi wa Gaza sasa wanategemea misaada kwa asilimia mia moja, huku vita vinavyoendelea vikiwasukuma wengi kwenye umaskini mkubwa.

Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, mashambulizi ya kijeshi ya muda mrefu yameharibu kabisa uchumi na miundombinu ya eneo hilo.

Mnamo Mei 7, 2025, kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa lilitoa tamko la pamoja likiitaka dunia ichukue hatua za haraka kusitisha mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na Israel huko Gaza.

Afrika Kusini imefungua kesi ya mauaji ya kimbari dhidi ya Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) na imesisitiza kuwa haitafuta kesi hiyo licha ya vitisho, mashinikizo na kukatiwa misaada na utawala wa Donald Trump.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha