16 Mei 2025 - 21:35
Source: Parstoday
Sasa hata Ufaransa yalaani jinai za kutisha za Israel

Jinai za Israel kwenye Ukanda wa Ghaza ni kubwa kiasi kwamba hata dola la kikoloni la Ufaransa ambalo ni moja ya waungaji mkono wakubwa wa Israel limeshindwa kuvumilia na limelaani jinai hizo likitaka kukomeshwa haraka na Netanyahu wawajibishwe na jamii ya kimataifa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Noel Barrot amesema hayo kwenye mahojiano na France 2 leo Ijumaa na kuongeza kwamba waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu lazima asikilize mwito wa pamoja wa jamii ya kimtaifa inayotaka kusitishwa mara moja vita katika Ukanda wa Ghaza.

Amesema: "Ufaransa imehamasika kufanya juhudi za kutatua mzozo wa kibinadamu huko Ghaza. Lakini Israel imejibu jitihada hizo kwa kufanya mashambulizi mapya na mabaya katika Ukanda wa Ghaza siku ya Alkhamisi, na kuua makumi ya watu kwa mujibu wa wafanyakazi wa misaada walioko ndani ya Ghaza.

Jana televisheni ya Al Jazeera ya Qatar ilinukuu vyanzo vya matibabu vya Palestina vikisema kwamba takriban watu 60, wakiwemo wanawake na watoto wadogo, wameuawa katika shambulio la Israel huko Khan Yunis kusini mwa Ukanda wa Ghaza pekee.

Ripoti zinasema kuwa, Wapalestina waliouawa shahidi na kujeruhi wamehamishiwa katika eneo la Nasser Medical Complex lililokuwa limejaa majeruhi na miili ya mashahidi, huku uhaba mkubwa wa vifaa vya matibabu ukiendela kushuhudiwa katika hospitali za Ukanda wa Ghaza.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, idadi ya mashahidi katika vita vya Ghaza tangu Oktoba 7, 2023, imepindukia 53,010 na idadi ya waliojeruhiwa imefikia 119,998. Idadi ya vifo tangu Machi 18, 2024, wakati Israel ilipoanza tena kuishambulia Ghaza imefikia mashahidi 2,876 huku Wapalestina 7,957 wakijeruhiwa. Huko nyuma Ufaransa iliunga mkono kibubusa jinai za Israel lakini kadiri maafa ya kibinadamu yalivyozidi, hatua kwa hatua ilijiunga na wakosoaji wa Tel Aviv.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha