4 Machi 2016 - 19:25
Ayatullah Waidh Tabasiy afariki dunia

Ayatullah Waidh Tabasiy ambaye pia alikuwa mwakilishi wa kiongozi mwadhamu wa mapinduzi ya kiislamu ya Iran katika mkoa wa Khurasani Razaviy amefariki dunia leo Ijumaa mkoani humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Ayatullah Haji sheikh Abasi Waidh Tabasiy ambaye pia alikuwa mwakilishi wa kiongozi mwadhamu wa mapinduzi ya kiislamu katika mkoa wa Khurasani Razaviy nchini Iran amefariki dunia alfajiri ya leo Ijumaa katika mji wa Mashhad.
Shughuli za mazishi ya Ayatullah Abasi Waidh Tabasiy yatafanyika kesho saa tatu asubuhi kutoka karibu na maktaba ya Imam Riza (a.s) na kuzikwa pembeni mwa kaburi la Imam Riza (a.s) katika mji wa Mashhad nchini Iran.
Kwa ajili ya wananchi waweze kushiriki kwa wingi katika mazishi ya mwanazuoni huyo kesho siku ya Jumamosi idara zote hata vituo vya mafunzo hazitafunguliwa katika mkoa huo.

mwisho wa Habari/290