28 Machi 2016 - 18:37
Papa alaani shambulio la Pakistan

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amelaani shambulizi la bomu lililofanywa na wanamgambo wa Kiislamu wa itikadi kali wa dhehebu la Sunni wahabia linalodhaminiwa na Saudia arabia na kuua zaidi ya watu 100 nchini Pakistan

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amelaani shambulizi la bomu lililofanywa na wanamgambo wa Kiislamu wa itikadi kali wa dhehebu la Sunni wahabia linalodhaminiwa na Saudia arabia na kuua zaidi ya watu 100 nchini Pakistan wengi waliouwawa wakiwa ni wakristo ambao ndio walikuwa walengwa wa shambulizi hilo. Kiongozi huyo wa kanisa katoliki amekitaja kitendo hicho kuwa cha kutisha na kuitaka serikali ya nchi hiyo kuwalinda waumini wa dini za waliowachache. Akiwahutubia maelfu ya watu katika uwanja wa kanisa la st Peter hii leo Jumatatu ya pasaka papa amesema Pakistan imeshuhudia umwagikaji mkubwa wa damu uliotokana na mashambulizi ambayo yamechukua uhai wa watu wengi wasiokuwa na hatia wengi wakiwa ni watu kutoka jamii ya wakristo waliowachache nchini humo. Kadhalika ametowa mwito kwa serikali na sekta zote nchini Pakistan kuchukua jitihada za kurudisha usalama na utulivu katika jamii na hasa kwa wale kwa jamii ya watu wenye dini za waliowachache.

Mwisho wa habari/ 291